FAO: Uhaba wa chakula katika nchi nyingi duniani unatia wasiwasi
(last modified Fri, 08 Dec 2017 07:50:23 GMT )
Dec 08, 2017 07:50 UTC
  • FAO: Uhaba wa chakula katika nchi nyingi duniani unatia wasiwasi

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limebainisha wasiwasi wake kuhusu uhaba wa chakula katika nchi nyingi duniani.

Fao imetangaza kuwa ukame, mafuriko na kushtadi mizozo kumesababisha kukosekana uthabiti katika uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za chakula licha ya kuongezeka uzalishaji wa chakula kimataifa. 

Takwimu za hivi karibuni kuhusu uzalishaji wa kilimo na bidhaa za chakula za shirika la Fao zinaonyesha kuwa nchi 37 zikiwemo 29 za Kiafrika zinahitaji msaada mkubwa wa chakula. 

Ukame nchini Sudan Kusini 

Maafisa wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa wanasema kuwa kuendelea machafuko kaskazini mwa Nigeria, Sudan Kusini, Yemen na pia kuwepo tatizo la njaa huko Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Syria pia ni moja ya sababu kuu zinazopelekea kukosekana usalama wa kutosha wakati wa kuandaa na kusambaza bidhaa za chakula katika nchi hizo na katika maeneo mengine yaliyoathiriwa na hali ya mchafukoge duniani.

  

Tags