Palestina yazitaka nchi za Afrika kukata uhusiano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46518-palestina_yazitaka_nchi_za_afrika_kukata_uhusiano_na_israel
Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina ameziomba nchi za bara la Afrika zitazame upya uhusiano wao na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 02, 2018 09:17 UTC
  • Palestina yazitaka nchi za Afrika kukata uhusiano na Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina ameziomba nchi za bara la Afrika zitazame upya uhusiano wao na utawala haramu wa Israel.

Riyad al-Maliki ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika unaofanyika Nouakchott nchini Mauritania amesema kuwa, kadhia ya Palestina ndiyo msingi wa kuwepo amani eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla na ametilia mkazo udharura wa nchi za Afrika kuonesha mshikamano wao na taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amewaomba viongozi wa nchi za Kiafrika kushikamana na msingi na malengo ya Umoja wa Afrika ya kupinga ubaguzi kwa kutazama upya uhusiano wao na utawala bandia wa Israel 

Al Maliki ameashiria uhalifu na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel huko Palestina kwa kipindi cha miaka 70 sasa na amewaomba viongozi wa nchi za Afrika kushirikiana na pande zote za kimataifa katika kutayarisha mazingira mazuri ya kukamatwa na kuhukumiwa watenda jinai wa utawala huo. 

Amesema kuwa uungaji mkono kwa taifa la Palestina unapaswa kudumishwa hadi nchi hiyo itakapokuwa huru na kuunda dola huru la Palestina, mji mkuu wake ukiwa Baitul Muqaddas.