Guterres atahadharisha kuhusu athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa
(last modified Tue, 11 Sep 2018 11:02:10 GMT )
Sep 11, 2018 11:02 UTC
  • Guterres atahadharisha kuhusu athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa na gesi chafu ni tishio la moja kwa moja kwa walimwengu.

António Guterres ametahadharisha kwamba, dunia inakabiliwa na tishio la kuwepo kwake na kuna ulazima wa kubadili mwenendo wa kutumia nishati ya fosili hadi mwaka 2020 na kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa. 

Guterres pia amekemea ukosefu wa uongozi wa dunia katika suala la kuzuia ongezeko la joto la dunia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasiwasi wake kutokana na kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa na kusema kuwa: Watu katika maeneo mbalimbali ya dunia wanasumbuliwa na wimbi la ongezeko la joto ambalo halijawahi kushuhuudiwa, na joto kali linateketeza maeneo mbalimbali na matufani na mafuriko yanaongezeka na kusababisha vifo na uharibifu. 

Ongezeko la joto la dunia linasababisha maafa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, kwa miongo kadhaa sasa wasomi wamekuwa wakitahadharisha kuhusu ongezeko la joto la dunia lakini baadhi ya viongozi wa nchi wanapuuza tahadhari hizo na wachache sana wamechukua hatua kwa mujibu wa maoni ya wataalamu.

  António Guterres amesisitiza kuwa, kuna udharura wa kusitisha utegemezi wa nishati ya fosili haraka iwezekanavyo na badala yake kutumia nishati ya maji, upepo na jua. 

Tags