Chama cha Labour: Uingereza iache kuiuzia silaha Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48398-chama_cha_labour_uingereza_iache_kuiuzia_silaha_israel
Chama cha Labour cha nchini Uingereza kimeitaka serikali ya nchi hiyo kuacha kuuzia silaha utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 26, 2018 04:52 UTC
  • Chama cha Labour: Uingereza iache kuiuzia silaha Israel

Chama cha Labour cha nchini Uingereza kimeitaka serikali ya nchi hiyo kuacha kuuzia silaha utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika mkutano wake, chama cha Labour kinyume na sera za Washington, kimetaka kuzidishwa misaada ya fedha ya London kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA). Katika sehemu nyingine ya hatua zao za kuipinga Israel, wabunge hao wa chama hicho wamelaani hatua ya utawala wa Kizayuni ya kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji wa Kipalestina huko Ghaza kwa kupiga kura za ndio. 

Hujuma za Israel dhidi ya waandamanaji wa Kipalestina Ghaza

Wabunge wa chama cha Labour nchini Uingereza jana walipiga kura hizo za ndio huku bendera za Palestina zikipeperushwa katika ukumbi wa mkutano.

Hali ya kibinadamu huko Ghaza ni mbaya sana kutokana na kuendelea mzingiro wa kiuchumi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya eneo hilo na kukatwa misaada ya Marekani kwa Wapalestina. 

Ukanda wa Ghaza uko chini ya mzingiro wa anga, nchi kavu na baharini uliowekwa na Israel tangu mwaka 2006 huku wakazi wa eneo hilo wakikabiliwa na tatizo kubwa la mafuta, chakula na madawa. Aidha mashambulizi makubwa ya kikatili ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza hadi sasa yameuwa shahidi na kujeruhi maelfu ya raia wa Palestina.