Lavrov: Russia imejiandaa kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51447-lavrov_russia_imejiandaa_kukabiliana_na_siasa_za_kibeberu_za_magharibi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema kuwa Moscow imejiandaa kukabiliana na siasa za kutwisha za madola ya Magharibi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 09, 2019 21:47 UTC
  • Lavrov: Russia imejiandaa kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amesema kuwa Moscow imejiandaa kukabiliana na siasa za kutwisha za madola ya Magharibi.

Lavrov amesema kuwa njama za kutaka kudhibiti siasa za kigeni za nchi nyingine zimefeli na kwamba jamii ya kimataifa imechoshwa na siasa za vitisho, vikwazo, mashinikizo na kueneza habari zisizo na ukweli dhidi ya upande mwingine.

Ameashiria msimamo hasi wa madola ya Magharibi hususan Marekani kuihusu Russia na kuongeza kwamba, hii si mara ya kwanza ambapo Wamagharibi wanakumbwa na maradhi la kujiona bora na kuwa juu ya sheria. Ameyasihi madola ya Magharibi yasisahau ibra za kihistoria.

Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza kwamba, jitihada zinazofanywa kwa ajili ya kuilazimisha Moscow ichukue maamuzi na kupanga siasa zake za nje kwa mujibu wa matakwa ya Marekani na Wamagharibi zimefeli na kushindwa.

Mahusiano ya Marekani na Umoja wa Ulaya na Russia yamezorota zaidi katika miezi ya hivi karibuni kutokana na hali ya ya Ukraine na kadhalika hatua ya kufukuzwa wanadiplomasia wa Russia kutoka katika nchi hizo za Magharibi.