Maduro aagiza kusimamiwa viwanja vya ndege katika mji mkuu wa Venezuela
(last modified Wed, 08 May 2019 12:14:11 GMT )
May 08, 2019 12:14 UTC
  • Maduro aagiza kusimamiwa viwanja vya ndege katika mji mkuu wa Venezuela

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela amesema kuwa serikali ya nchi hiyo itasimamia viwanja vitatu vya ndege vilivyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo kufuatia agizo la Rais wa nchi hiyo.

Nestory Reverol ameeleza kuwa serikali ndiyo itakayosimamia kikamilifu viwanja vitatu vya ndege katika mji mkuu Caracas kufuatia agizo la Rais Nicolaus Maduro. Hatua hiyo imechukuliwa ili kuweza kutekeleza hatua stahiki za kuzuia shughuli zozote zilizo kinyume cha sheria. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Venezuela ameongeza kuwa viongozi wa serikali watazifanyia ukarabati idara za polisi ya kimataifa (Interpol), idara ya uchunguzi wa jinai na masuala ya mipaka, idara ya kudhibiti madawa ya kulenya na ile ya wahamiaji katika viwanja hivyo vya ndege. 

Nicolaus Maduro, Rais halali wa Venezuela

Kwa kuwaunga mkono wapinzani vibaraka na kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela; Marekani na waitifaki wake zimeazimia kuiangusha serikali halali ya nchi hiyo ambayo imeonyesha waziwazi msimamo wake dhidi ya Washington. Kuhusiana na suala hilo, njama ya mapinduzi ya wiki iliyopita iliyotekelezwa na wapinzani vibaraka wa Washington dhidi ya serikali halali ya Rais Maduro imeambulia patupu, hata hivyo viongozi wa Marekani akiwemo John Bolton Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani siku zote amekuwa akitoa vitisho vya kuishambulia kijeshi Venezuela. 

  

Tags