Wapiganaji wa Muqawama nchini Iraq washambulia ngome za Israel
(last modified Fri, 25 Oct 2024 06:47:51 GMT )
Oct 25, 2024 06:47 UTC
  • Wapiganaji wa Muqawama nchini Iraq washambulia ngome za Israel

Wapiganaji wa Harakati  Mapambano ya Kiislamu (muqawama) nchini Iraq wametangaza kutekeleza oparesheni mpya dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Harakati hiyo ambayo inajumuisha makundi kadhaa ya muqawama nchini Iraq imetangaza Ijumaa asubuhi kwamba ndege zake zisizo na rubani zilishambulia ngome muhimu za Israel katika sehemu ya kusini ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq imeongeza kuwa pia imefanya mashambulizi mawili mfululizo ya ndege zisizo na rubani kwenye bandari ya Eilat inayokaliwa kwa mabavu na Israel ambayo jina lake asili la Kipalestina ni Umm Al-Rashrash.

Imebainisha kuwa operesheni hizo ni za kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na Lebanon.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq imesisitiza kuwa, mashambulizi hayo pia ni katika kujibu mauaji yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wakiwemo wanawake, watoto na wazee katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu.

Wapiganaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu wameapa kuendeleza oparesheni zao dhidi ya utawala haramu wa  Israel kwa nguvu zaidi maadamu utawala huo unaendeleza mauaji ya kimbari huko Gaza.