Zarif: Vikwazo vya Marekani vimevuruga mfumo wa dunia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53681-zarif_vikwazo_vya_marekani_vimevuruga_mfumo_wa_dunia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya Marekani vinalenga kuvuruga mfumo na nidhamu ya kimataifa.
(last modified 2024-06-10T09:25:34+00:00 )
May 24, 2019 07:09 UTC
  • Zarif: Vikwazo vya Marekani vimevuruga mfumo wa dunia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya Marekani vinalenga kuvuruga mfumo na nidhamu ya kimataifa.

Mohammad Javad Zarif aliyasema hayo Alhamisi alipozungumza na waandishi habari  mara baada ya kuwasili Islamabad, mji mkuu wa Pakistan. Zarif ameongeza kuwa, kufanya mashauriano na nchi jirani kuhusu hali mbaya katika eneo ni jambo la dharura.

Hali kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria hatua za kibabe za Marekani katika kulazimisha vikwazo dhidi ya Iran na China na kusema: "Iwapo jamii ya kimataifa itaruhusu hatua kama hizo ziendelee, basi mfumo wa mawasiliano duniani utakuwa mikononi mwa watu ambao hawafungamani na sheria yoyote."

Zarif ameendelea kusema ni kwa sababu hii ndio Iran inawataka majirani zake na nchi zote duniani zichukue hatua za kukabiliana na vikwazo vya Marekani kwa ajili ya kulinda usalama wa dunia na maslahi yao.

Marekani imetuma manoari zake za kivita katika eneo la Asia Magharibi na kuhatarisha usalama wa eneo hilo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema eneo la Asia Magharibi hivi sasa liko katika hali mbaya na hatua hatari zinachukuliwa, hivyo kuna haja ya nchi jirani kushauriana.

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana aliwasili Islamabad, Pakistank ikiwa ni muendelezo wa safari zake za hivi karibuni za kutembelea nchi muhimu za bara Asia.