UN yataka kuongezwa muda askari wake wa Sahara Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i5443-un_yataka_kuongezwa_muda_askari_wake_wa_sahara_magharibi
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuongezewa muda wa kuhudumu askari wa kulinda amani wa umoja huo katika eneo la Sahara Magharibi MINURSO, akionya kuwa, iwapo vikosi hivyo vitaondolewa kikamilifu, eneo hilo litakuwa katika hatari ya kushuhudia migogoro zaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 20, 2016 03:20 UTC
  • UN yataka kuongezwa muda askari wake wa Sahara Magharibi

Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuongezewa muda wa kuhudumu askari wa kulinda amani wa umoja huo katika eneo la Sahara Magharibi MINURSO, akionya kuwa, iwapo vikosi hivyo vitaondolewa kikamilifu, eneo hilo litakuwa katika hatari ya kushuhudia migogoro zaidi.

Ki-moon amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa vikosi hivyo kwa mwaka mmoja zaidi, ili kudumisha amani na kuzuia uwezekano wa kupanuka mgogoro uliopo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki ijayo linatazamiwa kupiga kura kuamua iwapo vikosi hivyo vitaongezewa muda au la. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameahidi kuwa umoja huo utaendelea na jukumu lake la kuutafutia suluhisho mgogoro wa karibu miongo minne kati ya harakati ya Polisario inayotaka kujitenga Sahara Magharibi na Morocco bila kuegemea upande wowote.

Morocco imekuwa ikisisitiza kuwa, iwapo kura ya maoni itaitishwa na eneo la Sahara Magharibi kujitenga na kujitangazia uhuru wake, yumkini nchi hiyo ya Kiarabu ikashuhudia migogoro zaidi katika siku zijazo.