Raia wa Venezuela wamzomea Juan Guaidó, alazimika kufuta hotuba yake
(last modified Sun, 30 Jun 2019 04:44:00 GMT )
Jun 30, 2019 04:44 UTC
  • Raia wa Venezuela wamzomea Juan Guaidó, alazimika kufuta hotuba yake

Raia wa Venezuela wamemlazimisha Juan Guaidó kiongozi wa upinzani afutilie mbali hotuba yake baada ya kumzomea na kuonyesha upinzani dhidi yake.

Guaidó ambaye ni kiongozi wa upinzani anayepata uungaji mkono kutoka Marekani na nchi nyingine za Magharibi alikumbwa na hali hiyo wakati alipokuwa ameingia katika kanisa Katoliki la Saint Peter katika mji wa pwani wa La Guaira ambapo idadi kubwa ya wakazi wa mji huo walijitokeza na kuanza kupiga nara dhidi yake. Katika safari hiyo Guaidó alikuwa amepanga kutoa hotuba kabla ya kuingia kanisa hapo ambapo watu walikusanyika na kupiga nara za 'haini' kumlenga mwanasiasa huyo. Aidha mpinzani huyo hakuweza pia kuhutubia kanisani kutokana na malalamiko ya wananchi dhidi yake.

Wananchi wakiandamana kumpinga Juan Guaidó

Machafuko na ghasia nchini Venezuela zilishtadi baada ya Juan Guaidó kujitangaza kuwa rais wa muda wa nchi hiyo kuanzia mwezi Januari mwaka huu. Katika uwanja huo serikali za Magharibi zimekuwa zikitangaza wazi kumuunga mkono kiongozi huyo wa upinzani kwa lengo la kutaka kumuondoa madarakani Nicolás Maduro, rais halali aliyechaguliwa na wananchi. Mkabala na madola hayo ya Maghharibi, nchi nyingi kama vile Russia, China, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afrika Kusini zimetangaza kumuunga mkono rais anayetambuliwa kikatiba, yaani Rais Nicolás Maduro.

Tags