John Bolton aingilia tena masuala ya ndani ya Venezuela
(last modified Wed, 07 Aug 2019 01:19:40 GMT )
Aug 07, 2019 01:19 UTC
  • John Bolton aingilia tena masuala ya ndani ya Venezuela

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani amesema kuwa Washington inapinga kufanyika uchaguzi mpya nchini Venezuela madhali Rais wa sasa wa nchi hiyo ataendelea kusalia madarakani.

John Bolton amedai katika kikao huko Lima mji mkuu wa Peru kuwa mazungumzo yanayaoendelea kati ya serikali ya Rais Nicolas Maduro na mrengo wa upinzani katika kisiwa cha Barbados hayako jadi na akasema serikali ya Caracas inapoteza wakati tu katika mazungumzo hayo. Bolton ameyasema hayo katika hali ambayo pande mbili hizo yaani serikali ya Venezuela na wapinzani zinaendelea kufanya mazungumzo ili kujitoa katika mkwamo wa kisiasa ulioiathiri nchi hiyo ya Amerika ya Latini. 

Rais Donald Trump wa Marekani juzi Jumatatu alisaini dikrii akiamuru kuzuiliwa fedha za Venezuela zilizoko Marekani ikiwa ni muendelezo wa hatua zake za uhasama dhidi ya serikali ya Caracas. Juan Guaido kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Jumatano tarehe 23 Januari mwaka huu huku akiungwa mkono wazi wazi na Marekani na waitifaki wake wengine alijitangaza kuwa Rais wa Venezuela hatua ambayo ilitajwa na serikali na wananchi wa nchi hiyo kuwa mapinduzi dhidi ya Rais halali Nicolas Maduro. 

Rais halali wa Venezuela, Nicolas Maduro 
 

 

Tags