Rais Vladimir Putin wa Russia ataka kupunguzwa ulizalishaji wa mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60154-rais_vladimir_putin_wa_russia_ataka_kupunguzwa_ulizalishaji_wa_mafuta
Rais Vladimir Putin wa Russia amewataka wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani kupunguza ulizashaji wa mafuta kwa lengo la kuimarisha bei.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 03, 2020 23:56 UTC
  • Rais Vladimir Putin wa Russia ataka kupunguzwa ulizalishaji wa mafuta

Rais Vladimir Putin wa Russia amewataka wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani kupunguza ulizashaji wa mafuta kwa lengo la kuimarisha bei.

Rais Putin ameyasema hayo kwenye kikako kilichofanyika kwa njia ya video ambapo sambamba na kusisitizia umuhimu wa kushushwa kiwango cha uzalishaji wa mafuta hadi kufikia mapipa milioni 10 kwa siku kutoka kwa wazalishaji wakubwa wa nishati hiyo ikiwemo Marekani na Saudia, amesema kuwa, hatua zote ni lazima zichukuliwe kwa namna shirikishi. Ameongeza kuwa, hali ya soko la mafuta duniani ni mbaya sana na virusi vya Corona vimeathiri uchumi wote wa dunia. Ameendelea kufafanua kuwa suala hilo ndilo limesababisha kupungua kiwango cha uhitaji kutoka kwa watumiaji wake. Kwa ajili hiyo pande zote wakiwemo washirika wa Russia wanafahamu ukweli huu kwamba suala la kupunguzwa kiwango cha uzalishaji wa mafuta hadi kufikia chini ya kile kilichokuwepo kabla ya mgogoro, ni jambo muhimu.

Rais Vladimir Putin wa Russia 

Amesisitiza kuwa serikali ya Moscow iko tayari kushirikiana na wazalishaji wa mafuta ikiwemo Marekani kwa lengo la kuleta mlingano wa bei katika soko la dunia. Makubaliano ya mafuta kati ya wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) kuhusu kupunguza uzalishaji wa kiwango cha mapipa milioni moja na nusu kwa siku, yalifikia tamati Aprili mosi, baada ya upinzani wa serikali ya Moscow kwa suala la kupunguzwa uzalishaji zaidi kutokana na taathira ya Corona. Baada ya hapo Saudia ilitangaza kuongeza kiwango cha ulizashaji wake wa nishati hiyo muhimu kufikia mapipa milioni 13 kwa siku, suala ambalo limepelekea kushuka kwa bei ya mafuta duniani.