Russia yatangaza mshikamano wake na watu wa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60844-russia_yatangaza_mshikamano_wake_na_watu_wa_iran
Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amewatumia barua viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akitangaza mshikamano wake na raia wa nchi hii kutokana na mapambano yao makubwa dhidi ya vikwazo haramu na vya upande mmoja vya Marekani katika mazingira ya sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2020 22:19 UTC
  • Russia yatangaza mshikamano wake na watu wa Iran

Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amewatumia barua viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akitangaza mshikamano wake na raia wa nchi hii kutokana na mapambano yao makubwa dhidi ya vikwazo haramu na vya upande mmoja vya Marekani katika mazingira ya sasa.

Lavrov alituma ujumbe huo wa maandishi kwa Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambapo ametangaza upinzani wake dhidi ya mienendo iliyo dhidi ya binaadamu ya Marekani katika uga wa kushadidisha vikwazo vyake haramuu na vya upande mmoja  dhidi ya Tehran. Katika barua hiyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza kuwa, serikali ya Moscow inavichukulia vikwazo hivyo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran kuwa kinyume cha sheria. Amesema kuwa nchi yake inaitaka Marekani kufuta vikwazo hivyo.

Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia

Kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezitaka nchi za Ulaya Magharibi pia kuacha kutishwa na vitisho vya Washington na badala yake ziendelee kuamiliana vyema na Iran. Ameashiria uhusiano mwema uliopo kati ya Iran na Russia, na kusisitiza kuwa katika siku zijazo pia Moscow itaendelewa kuwaunga mkono watu wa Iran. Hii ni katika hali ambayo Umoja wa Mataifa, asasi za kimataifa na nchi nyingi za dunia, zimetaka kusimamishwa vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran. Vikwazo vya Marekani vinazuia kutumwa zana za tiba na madawa ya dharura nchini Iran.