Jun 02, 2020 08:05 UTC
  • Rais Tayyip Erdoğan: Misikiti yote mjini Athens, Ugiriki, imeharibiwa

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa misikiti yote mjini Athens, mji mkuu wa Ugiriki, imeharibiwa kwa amri ya viongozi wa nchi hiyo.

Rais Erdoğan ameyasema hayo mjini Istanbul na kuongeza kwamba, hakuna msikiti hata mmoja uliobakia salama mjini Athens. Akikosoa vikali miamala ya baadhi ya nchi za Magharibi kuwahusu Waislamu wanaoishi nchi hizo, rais wa Uturuki ameongeza kuwa, katika vipindi vilivyopita Waislamu hawakuwa na lengo la kuziteka nchi bali lengo lao kuu lilikuwa ni kuziteka nyoyo za watu. Migogoro ya kidiplomasia kati ya Ugiriki na Uturuki iliibuka baada ya kukosolewa suala la kusomwa Qur'ani katika mji wa kihistoria wa Hagia Sophia unaopatikana mjini Istanbul.

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki

Serikali ya Athens inadai kwamba, kufanyika marasimu hayo ya kidini katika msikiti wa kihistoria wa Hagia Sophia, ni kinyume na hati ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) ambayo inasisitiza kulindwa maeneo ya kihistoria. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki pia sambamba na kutupilia mbali tuhuma hizo za Ugiriki imeitaka serikali ya Athens kuacha kuharibu misikiti ya Waislamu badala ya kutoa tuhuma zisizo na msingi.

Tags