Maandamano ya kuunga mkono Palestina yafanyika Italia
Watu wa Italia wameshiriki katika maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Roma kwa lengo la kutangaza uungaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina sambamba na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Iran Press, waandamanaji ambao walikuwa wamebeba bendera za Palestina walitoa nara dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huku wakilaani vikali hujuma za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza na Msikiti wa Al Aqsa.
Waandamanaji hao Wataliaoni wametaka taasisi za kimataifa ziuwekee vikwazo vya kiuchumi utawala wa Kizayuni wa Israel.
Wiki tatu zilizopita pia maelfu ya watu wa Italia walishiriki katika maandamano mjini Roma na kutangaza kufungamana na taifa na mapambano ya Palestina.
Waandamanaji hao walilaani vikali hujuma ya siku 12 ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza iliyoanza Mei 10 na kupelekea Wapalestina 248 kuuawa shahidi wakiwemo watoto 69, wanawake 39 na wazee 17 huku wengine 1,910 wakijeruhiwa.
Baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel ililazimika kukubali usitishwaji vita baada ya oparesheni za ulipizaji kisasi za makundi ya muqawama ya Palestina ambayo yalivirumisha mamia ya makombora katika makazi ya Wazayuni.