"Saudi Arabia ni Benki ya Daesh (ISIS)"
https://parstoday.ir/sw/news/world-i7138-saudi_arabia_ni_benki_ya_daesh_(isis)
Maandamano yamefanyika nje ya Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Berlin, Ujerumani ambapo washiriki wameilaani Saudia kwa kuendelea kutoa misaada kwa kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 15, 2016 09:45 UTC

Maandamano yamefanyika nje ya Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Berlin, Ujerumani ambapo washiriki wameilaani Saudia kwa kuendelea kutoa misaada kwa kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.

Waandamanaji hao waliokuwa na hasira wamelaani uungaji mkono wa Saudia kwa magaidi huko Syria, Iraq, Yemen na nchi zingine duniani.

Katika kuonyesha namna Saudi Arabia inavyounga mkono makundi ya kigaidi ikiwemo ISIS, waandamanaji hao ambao waliandamana jana usiku walitumia mwangaza wa laser kuibua bendera ya kundi la kigaidi la ISIS na juu yake ikiwa na maneneo ya 'Benki ya Daesh' na kuelekeza mwangaza huo katika jengo la ubalozi wa Saudia mjini Berlin.

Maandamano hayo ni ishara ya wazi kuwa waliowengi barani Ulaya wanaamini kuwa utawala wa Saudia ni muungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi.