Lavrov: Russia inapinga kuwepo wanajeshi wa Marekani katikati mwa Asia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i73906-lavrov_russia_inapinga_kuwepo_wanajeshi_wa_marekani_katikati_mwa_asia
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa, nchi hiyo inapinga suala la kupelekwa wanajeshi wa Marekani katika eneo la katikati mwa Asia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 25, 2021 03:23 UTC
  • Sergey Lavrov
    Sergey Lavrov

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa, nchi hiyo inapinga suala la kupelekwa wanajeshi wa Marekani katika eneo la katikati mwa Asia.

Sergey Lavrov amesema kuwa, Moscow haitaki kuwepo wanajeshi wa Marekani katika nchi za Katikati mwa Asia hadi kusini mwa mipaka ya Russia. 

Awali Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Russia alikuwa amesema kuwa, hakuna hata nchi moja ya Asia ya Kati iliyokubali kuwepo wanajeshi wa Marekani katika ardhi yake. 

Tayari nchi za kanda hiyo zimepinga fikra ya kuwepo kambi za kijeshi za Marekani katika nchi hizo sambamba na upinzani unaoendelea kutangazwa na Russia dhidi ya kuwepo wanajeshi wa nchi za Magharibi hususn Marekani na NATO katika maeneo ya Asia ya Kati na Caucasus Kusini.

Katika miaka ya karibuni Marekani na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) zimekuwa zikifanya mikakati ya kujenga vituo vya majeshi yao katika nchi mbalimbali  hususan kandokando ya mipaka ya Russia.