Iran yalaani mauaji ya Waislamu msikiti wa Ijumaa Kunduz huko Afganistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i75524-iran_yalaani_mauaji_ya_waislamu_msikiti_wa_ijumaa_kunduz_huko_afganistan
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mauaji ya makumi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika hujuma ya kigaidi iliyolenga ibada ya Swala ya Ijumaa mapema leo katika mji wa Kunduz huko kaskazini mashariki mwa Afghanistan.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Oct 08, 2021 13:42 UTC
  • Iran yalaani mauaji ya Waislamu msikiti wa Ijumaa Kunduz huko Afganistan

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani mauaji ya makumi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia katika hujuma ya kigaidi iliyolenga ibada ya Swala ya Ijumaa mapema leo katika mji wa Kunduz huko kaskazini mashariki mwa Afghanistan.

Saeed Khatbzadeh amelaani shambulio hilo la kigaidi ambalo limeua Waislamu wasiopungua 60 walikuwa wakishiriki Swala ya Ijumaa msikitini na kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulizi hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inalaani ugaidi katika sura zake zote na magaidi wote. 

Vyombo vya usalama nchini Afghanistan vimethibitisha kuwa, idadi ya waliopoteza maisha katika hujuma hiyo ya kigaidi imefikia watu 60 na kwamba wengine zaidi ya 107 wamejeruhiwa.

Maiti za Waislamu ndani ya msikiti wa Swala ya Ijumaa, Kunduz

Naibu Waziri wa Habari na Utamaduni wa Taliban, Zabihullah Mujahid, amesema, kikosi maalumu cha serikali kimetumwa eneo la Kunduz kuchunguza tukio hilo.

Hadi tunatayarisha habari hii Hakukuwa na kundi lolote lililotoa madai ya kuhusika na shambulio hilo, lakini kumekuwa na mashambulio kadhaa nchini humo katika wiki za hivi karibuni, ambayo kundi lenye mfungamano na genge la kitakfiri la Daesh limedai kuhusika na baadhi yake.