Skuli za wasichana zafunguliwa tena katika mkoa wa Herat, Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i76640-skuli_za_wasichana_zafunguliwa_tena_katika_mkoa_wa_herat_afghanistan
Skuli za wasichana katika mkoa wa Herat nchini Afghanistan zimefunguliwa tena.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 07, 2021 12:06 UTC
  • Skuli za wasichana zafunguliwa tena katika mkoa wa Herat, Afghanistan

Skuli za wasichana katika mkoa wa Herat nchini Afghanistan zimefunguliwa tena.

Sabir Mash'al, mkuu wa baraza la walimu wa skuli za mkoa wa Herat ulioko magharibi mwa Afghanistan ametangaza kuwa, skuli za wasichana za mji wa Herat, makao makuu ya mkoa huo zimefunguliwa tena na akaongeza kwamba, karibuni hivi na katika miji na vitongoji vingine vya mkoa huo wa Herat, wasichana wataweza kurudi tena maskulini.

Sabir Mash'al amebainisha kuwa, kwa sasa hakuna mpaka wowote uliowekwa kwa ajili ya kufunguliwa tena mashule katika mkoa wa Herat na kwamba wanafunzi wa kike wa ngazi zote wanaweza kurudi madarasani.

Kwa muda wa takribani miezi mitatu sasa wavulana na walimu wa kiume wanaendelea kwenda mashuleni, lakini wanafunzi wa kike kuanzia darasa la saba pamoja na walimu wanawake wamelazimika kubakia majumbani.

Viongozi wa Taliban

Kufungwa kwa skuli za wanafunzi wa kike wa ngazi ya zaidi ya darasa la sita kumekabiliwa na wimbi kubwa la ukosoaji ndani na nje ya Afghanistan.

Kundi la Taliban, ambalo tarehe 15 Agosti lilishika hatamu za utawala nchini Afghanistan, linajaribu kuwatoa hofu na kuwapa hakikisho wananchi wa nchi hiyo na jamii ya kimataifa juu ya suala la kuheshimu haki za wanawake, hata hivyo hadi sasa halijatekeleza ahadi yake hiyo.../