WHO: Kampeni ya kutoa chanjo barani Afika inaenda mwendo wa kinyonga
-
Matshidiso Moeti
Shirika la Afya Duniani limetangaza kuwa, kuna uwezekano kwamba, itakuchua muda wa kufikia nusu ya pili ya mwaka 2024 ili bara la Afrika liweze kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa asilimia 70 ya jamii ya watu wa bara hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema" "katika hali ya sasa, yumkini Afrika isiweza kufikia lengo lake la kuchanja asilimia 70 ya watu wa bara hilo ifikapo Agosti 2024." Moeti amekariri wito wake kwa nchi tajiri kutoa chanjo ya Covid-19 kwa nchi za bara la Afrika.
Vilevile ameashiria kipindi kifupi cha kuisha muda wa matumizi wa baadhi ya chanjo za corona na matatizo mengine na kusema kuwa jumla ya dozi 910,000 za chanjo hiyo zimeisha muda wake katika takriban nchi 20 za Afrika.
Shaka na upinzani dhidi ya chanjo hiyo umesababisha kupungua idadi ya watu wanaochwanjwa nchini Afrika Kusini na katika mataifa mengine yenye chanjo za kutosha. Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika ametoa wito kwa serikali za nchi mbalimbali za Afrika kutoa elimu na taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu chanjo ya corona.
Jana Jumatano Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alitahadharisha kuwa kirusi cha corona aina ya Omicron sasa kinaenea kwa kasi ambayo haikushuhudiwa katika spishi nyinginge na kuna uwezeko Omicron ikawa tayari imeenea katika nchi nyingi duniani. Dakta Tedros Adhanom alisema nchi 77 duniani zimeripoti kuwa na maambukizi ya kirusi kipya cha Omicron.