Tufani kubwa yakata umeme wa makumi ya maelfu ya nyumba Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i79806-tufani_kubwa_yakata_umeme_wa_makumi_ya_maelfu_ya_nyumba_marekani
Kimbunga na mafuriko yaliyoripotiwa katika majimbo yasiyopungua matano nchini Marekani yamesitisha safari zaidi ya 6000 za ndege kutokana na upepo mkali, theluji na vimbunga vilivyoathiri ukanda wa pwani ya mashariki ya Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2022 00:35 UTC
  • Tufani kubwa yakata umeme wa makumi ya maelfu ya nyumba Marekani

Kimbunga na mafuriko yaliyoripotiwa katika majimbo yasiyopungua matano nchini Marekani yamesitisha safari zaidi ya 6000 za ndege kutokana na upepo mkali, theluji na vimbunga vilivyoathiri ukanda wa pwani ya mashariki ya Marekani.

Tovuti ya 25 ya Boston imeripoti kuwa kimbunga kikali pamoja na theluthi vilivyouathiri ukanda wa pwani ya mashariki nchini Marekani vimepelekea kusitishwa zaidi ya safari za ndege 5,600 nchini humo siku za Ijumaa na jana Jumapili. Juzi Jumamosi pia safari 4,800 za ndege zilisitishwa nchini Marekani kutokana na hali mbaya ya hewa. 

Shirika la habari la BBC pia limeripoti kuwa, tufani hiyo ni kati ya vimbunga vikali zaidi vya msimu wa baridi kali kuwahi kuikumba Marekani katika kipindi cha miaka minne ya karibuni.

Wakati huo huo  wataalamu wa hali ya hewa wameeleza kuwa tufani hiyo kali iliyoikumba Marekani ni mchanganyiko wa theluji na vimbunga vikali kutokana harakati ya Bahari ya Antlantic kuelekea katika pwani za Marekani kama New York na Massachusetts. 

Huduma ya umeme na safari za ndege zasitishwa katika baadhi ya majimbo nchini Marekani 

Kufuatia hali hiyo, majimbo ya Marekani yasiyopungua matano yako katika hali ya hatari huku makumi ya maelfu ya nyumba zikikosa huduma za umeme katika pwani ya mashariki ya nchi hiyo.