Wanachama kadhaa wa Umoja wa Ulaya wapinga vikwazo dhidi ya Russia
(last modified Mon, 29 Aug 2022 07:27:34 GMT )
Aug 29, 2022 07:27 UTC
  • Wanachama kadhaa wa Umoja wa Ulaya wapinga vikwazo dhidi ya Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland amesema kuwa, kuna wanachama kadhaa wa Umoja wa Ulaya wanapinga vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia.

Shirika la habari la Sputnik limemnukuu Péter Szijjártó akisema hayo na kuongeza kuwa, Poland haina hata hamu ya kuzungumzia vikwazo zaidi vya Magharibi dhidi ya Russia hususan linapokuja suala la mafuta na gesi. 

Mwezi Julai mwaka huu pia, Waziri Mkuu wa Poland alisema kwamba vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia vimezisababishia nchi za Ulaya matatizo mengi ya kiuchumi na kisiasa. Makali ya vikwazo hivyo kwa kweli vimeziathiri kwanza nchi za Ulaya zenyewe kabla ya hata Russia. 

Shirika la habari la Reuters la nchini Uingereza nalo limeripoti kuwa, kupanda bei ya nishati nchini humo kuna madhara yasiyofidika kwa baadhi ya familia, na maisha ya familia hizo yameingia hatarini kutokana na sera hizo.

Péter Szijjártó, Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland

 

Kwa upande wake, shirika la habari la IRIB limezinukuu duru za nchini Uingereza zikisema kuwa, wananchi wa nchi hiyo wamevamia vituo vya mafuta na kuviharibu ikiwa ni kulalamikia sera mpya za mafuta na gesi za serikali ya nchi hiyo ambazo zinamkandamiza mwananchi wa kawaida.

Harakati hizo za wananchi wa Uingereza zimefanyika katika hali ambayo juzi Jumamosi, serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuwa, kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu wa 2022, bei za umeme na gesi zitapanda kwa karibu mara mbili kwa watumiaji wa majumbani na matumizi ya familia.  

Sera hizo mpya za nishati za serikali ya Uingereza zinaonesha kuwa, kila familia ya nchi hiyo itakuwa inalipa Pound karibu elfu nne kwa ajili ya gesi na umeme kila mwaka  wakati hivi sasa kila familia inalipa karibu Pound 2,000 na tayari watu wanalalamikia ughali wa bidhaa hizo muhimu. Mwezi Aprili mwaka huu, yaani miezi michache tangu kuanza vita vya Ukraine, bei ya umeme ilipanda kwa asilimia 54 nchini UIngereza na kuziathiri familia 24 za nchi hiyo.

Tags