Sep 11, 2022 11:55 UTC
  • Mgogoro wa nishati wasababisha maandamano katika nchi za Ulaya

Miji kadhaa ya nchi za Ulaya imeshuhudia maandamano ya kulalamikia ongezeko la bei za nishati, huku mgogoro wa mafuta ya petroli na gesi ukiendelea kuyasumbua mataifa mengi ya bara Ulaya.

Maandamano makubwa ya Vizibao vya Njano yameshuhudiwa nchini Ufaransa, kulaani kupanda kwa bei za nishati katika nchi hiyo ya Ulaya.

Aidha maandamano kama hayo yameshuhudiwa katika mji mkuu wa Vienna, Austria na pia katika mji wa Naples nchini Italia. Habari zaidi zinasema kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Luigi Di Maio ameshambuliwa na waandamanaji waliokuwa na hasira na kumtaja kama 'msaliti'.

Waandamanaji jijini Vienna wamesikika wakipiga nara dhidi ya Umoja wa Ulaya, shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO, Chasela wa nchi hiyo, Alexander Schallenberg na mabwenyewe wanaofaidi kutokana na vita vya Ukraine.

Mgogoro wa nishati Ulaya waibua maandamano

Nchi za Ulaya, ambazo ziliamua kuiwekea Russia vikwazo vya kila aina ili kuishinikiza katika vita vya Ukraine, hivi sasa zinakabiliwa na mgogoro mkubwa wa nishati.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza mara kadhaa kuwa ipo tayari kuitatulia Ulaya matatizo yake ya nishati,  iwapo makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yatahuishwa.

Tags