Jun 17, 2016 07:06 UTC
  • Putin na Ban Ki-moon wajadili kadhia ya Syria

Rais Vladimir Putin wa Russia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon wamekutana na kujadili kadhia ya Syria.

Katika mazungumza hayo ambayo pia yamehudhuriwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria Staffan de Mistura, pande hizo zimejadiliana na kubadilishana mawazo juu ya utatuzi wa mgogoro wa Syria.

Kabla ya mazungumzo ya Ban Ki-moon na Rais Vladimir Putin wa Russia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikuwa tayari amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Sergei Lavrov. Pande hizo mbili zimesisitiza udharura wa kufanyika jitihada zaidi kwa ajili ya kupata utatuzi wa migogoro ya Syria, Yemen na Libya.

Mazungumzo hayo yamefanyika kandokando ya mkutano wa kimataifa wa kiuchumi huko Saint Petersburg unaohudhuriwa na ujumbe 800 za serikali na zisizo za serikali kutoka nchi mbalimbali duniani.

Tags