Russia: Ukraine imewashambulia raia kwa makombora ya Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i97322-russia_ukraine_imewashambulia_raia_kwa_makombora_ya_uingereza
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa jeshi la Ukraine limewashambulia raia kwa kutumia makombora ya Uingereza.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
May 13, 2023 21:58 UTC
  • Russia: Ukraine imewashambulia raia kwa makombora ya Uingereza

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa jeshi la Ukraine limewashambulia raia kwa kutumia makombora ya Uingereza.

Wizara ya Ulinzi ya Russia jana ilitangaza kuwa jeshi la Ukraine limetekeleza mashambulizi katika maeneo ya raia huko Luhansk kwa kutumia makombora ya masafa marefu ya Uingereza na kuwajeruhi watoto 6. Wizara ya Ulinzi ya Russia aidha imesisitiza kuwa jeshi la Ukraine limetumia makombora ya Cruz kwa jina la Storm Shadow kuwashambulia raia katika jimbo la Luhansk ambayo Uingereza iliipatia nchi hiyo kwa kisingizio cha kujiri vita nchini humo.

Taarifa hii imetolewa katika hali ambayo, huko nyuma serikali ya Uingereza iliipatia Ukraine makombora kadhaa ya Cruz ya masafa marefu aina ya Storm Shadow na mifumo kadhaa ya makombora ya M-270 ya kurushia roketi.  

Image Caption

Ni miezi 15 sasa ambako vita vinaendelea huko Ukraine huku vikiwa vimesababisha athari mbaya za kisiasa, kijeshi, kiuchumi na hata kiutamaduni. Wakati huo huo nchi za Magharibi zinaendelea kutuma silaha na zana mbalimbali za kijeshi nchini humo.  

Viongozi wa Russia, baadhi ya weledi wa mambo na vyombo vya habari vya Magharibi wamevitaja vita vya Ukraine kuwa ni vita vya niaba kati ya Magharibi na Russia. Russia imesema mara kadhaa kwamba hatua ya nchi za Magharibi ya kutuma silaha huko Ukraine inachochea vita na kuvifanya viendelee kwa muda mrefu sambamba na kusababisha athari zisizowezeza kutabirika.