EU: Vikwazo vya Marekani vinakanyaga sheria za kimataifa
(last modified Tue, 13 Jun 2023 07:33:52 GMT )
Jun 13, 2023 07:33 UTC
  • EU: Vikwazo vya Marekani vinakanyaga sheria za kimataifa

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema vikwazo vya Marekani mbali na kukiuka mamlaka ya kujitawala nchi nyingine duniani, lakini pia vinakanyaga sheria na kanuni za kimataifa.

Josep Borrell amesema hayo katika mahojiano na gazeti la The Straits Times la Malaysia ambapo amekosoa sera hiyo ya vikwazo ya Marekani dhidi ya mataifa mbali mbali duniani.

Borrell amesema kuna tofauti kubwa kati ya 'vikwazo' vinavyowekwa na Marekani na 'hatua za vizuizi' zinazchukuliwa na Ulaya na kueleza kuwa, hakuna neno 'vikwazo' kwenye hati za EU. 

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amefafanua kwa kusema, "Sera yetu ya vizuizi ni tofauti na vikwazo vya Marekani. Kwa mfano, hatuwezi kuilazimisha kampuni ya Indonesia kufungamana na sheria zetu (EU)." 

Borrell amesema sera ya vizuizi ya Umoja wa Ulaya inahusu kubana vitendo fulani kama vile kutonunua gesi ya Russia na kutoiuzia nchi hiyo vifaa vya kielektroniki inavyohitaji kuzalisha silaha.

US inatumia vikwazo kuziadhibu nchi zisizokubali kuburuzwa

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amewahi kukiri kuwa, sera ya mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi ya Marekani dhidi ya Iran imefeli na kugonga mwamba.

Hivi karibuni pia, Alena Douhan ambaye ni Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya athari mbaya za hatua za upande mmoja alisema kuwa, vikwazo vya upande moja vimedhoofisha uwezo wa kiutendaji wa UN na kuibua hofu katika ushirikiano wa kimataifa na utawala wa sheria. 

Tags