1
Maana ya Umoja na Mshikamano Baina ya Waislamu
Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh. Hamjambo na karibuni kuwa nami katika kipindi cha kwanza cha mfululizo wa makala maalumu za Wiki ya Umoja wa Kiislamu zinazokujieni kwa mnasaba wa sherehe za Maulidi na tukio muhimu la kuzaliwa Mtume wa rehma na upendo, Muhammad (saw) katika mwezi huu wa Mfunguo Sita .