Dec 14, 2024 02:26 UTC
  • Jumamosi, 14 Disemba, 2024

Leo ni Jumamosi 12 Mfunguo Tisa Jamadithani 1446 Hijria mwafaka na 14 Disemba 2024

Siku kama ya leo miaka 803 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria, alifariki dunia Abul Hassan Ali bin Abdu Samad Hamdani, mtambuzi wa lugha, fakihi na mfasiri wa Qur'ani katika karne ya 7 Hijria. Alizaliwa huko Sakha nchini Misri na akaondokea kuwa mashuhuri kwa lakabu ya Sakhawi. Akiwa na lengo la kujiendeleza kielimu, Abul Hassan Ali bin Abdu Samad alielekea Sham na kuishi Damascus katika Syria ya leo. Msomi huyo wa Kiislamu ameandika vitabu mbalimbali katika elimu za Tajweed, teolojia na hadithi. Baadhi tu ya vitabu vyake mashuhuri ni pamoja na al Jawahir na Sifrus Sa'ada.

Abul Hassan Ali bin Abdu Samad Hamdani,

 

Miaka 112 iliyopita inayosadifiana na tarehe 14 Disemba 1911, baada ya juhudi na jitihada za miaka mingi, hatimaye Ncha ya Kusini yaani South Pole ilivumbuliwa na kwa mara ya kwanza na wavumbuzi kadhaa waliwasili katika eneo hilo. Katika siku hii, Roald Amundsen baharia mashuhuri wa Kinorway aliyekuwa akishindana na Robert Falcon Scott wa Uingereza ili kuifikia ncha hiyo ya kusini, aliibuka mshindi na kuitundika bendera ya Norway katika ncha hiyo. Robert Falcon Scott akiwa na wenzake walikumbana na theluji kali wakati wanarejea na kupoteza maisha yao. 

Roald Amundsen

 

Katika siku kama ya leo miaka 74 iliyopita, yaani tarehe 24 Azar 1329 Hijiria Shamsia, alifariki dunia Hujjatul Islam Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani. Msomi na alimu huyo wa Kiirani aliyekuwa mmoja wa watoa waadhi na makhatibu mashuhuri katika zama zake alikuwa na azma na irada imara ya kueneza na kuwafikishia walimwengu maarifa ya Uislamu na ya Ahlul-Bait (as). Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani alikuwa akitoa mihadhara mjini Mash'had Iran na katika miji mingine na kadhalika katika Haram ya Imam Hussein (as) katika mji wa Karbala na Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) huko Najaf, Iraq. Hatimaye akiwa na umri wa takribani miaka 82 aliaga dunia katika siku kama ya leo na kuzikwa katika Haram ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (as) mjini Mash'had.

Hujjatul Islam Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani

 

 

Siku kama ya leo miaka 42 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 14 Disemba 1981 Bunge la utawala haramu wa Israel 'Knesset' liliiunganisha rasmi miinuko ya Golan ya huko Syria na ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu. Hatua hiyo ya kinyama ilikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa nchi za Kiislamu, Kiarabu pamoja na jamii ya kimataifa. Utawala dhalimu wa Israel uliikalia kwa mabavu miinuko hiyo ya Golan ya Syria katika vita baina yake na Waarabu mwaka 1967. 

Miinuko ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu

 

 

Katika siku kama ya leo miaka 27 iliyopita, makubaliano ya amani ya Bosnia yaliyojulikana kwa jina la "Dayton Peace Agreement" yaani Makubaliano ya Amani ya Dayton" yalithibitishwa kwa mara ya mwisho katika kikao kilichofanyika mjini Paris, Ufaransa. Makubaliano hayo ambayo yalifanyika kwa mashinikizo ya viongozi wa Marekani tarehe 21 Novemba 1995, yalitiwa saini na Marais wa wakati huo wa Bosnia Herzegovina, Serbia na Croatia. Mafanikio pekee ya makubaliano hayo kwa upande wa Waislamu, yalikuwa ni kuhitimishwa mauaji ya kinyama yaliyokuwa yakifanywa dhidi yao na  Waserbia. 

"Dayton Peace Agreement"   (Makubaliano ya Amani ya Dayton)