Dec 16, 2024 14:16 UTC
  • Jumatatu, 16 Disemba, 2024

Leo ni Jumatatu tarehe 14 Mfunguo Tisa Jamadithani 1446 Hijria mwafaka na tarehe 16 Disemba 2024.

Siku kama ya leo miaka 941 aliyopita, alifariki dunia msomi na mtaalamu wa fiq'hi wa Kiirani, Abu Hamid Muhammad Ghazali Tusi, maarufu kwa jina la Imam Muhammad Ghazali.

Baada ya kuaga dunia baba yake, yeye na kaka yake, Ahmad walilelewa na Ahmad bin Radkani. Ghazali alisoma elimu ya fiq'hi kutoka kwa Abu Nasri Ismail na baada ya kufikia umri wa miaka 28 alikuwa mmoja wa wasomi wakubwa wa Kiislamu katika elimu hiyo.

Umaarufu wa Imam Muhammad Ghazali ulipelekea kiongozi wa Iraq wakati huo Khoja Nidham al-Mulk kumwalika msomi huyo ili aende mjini Baghdad kwa ajili ya kufundisha. Hatimaye alirejea Iran na kujishughulisha na masuala ya ualimu.

Kabla ya kurejea Iran, Imam Muhammad Ghazali alipata kuandika vitabu vya thamani kama "Ihyau Ulumud Din," "Kemia ya Saada" na "Nasaha za Wafalme."

Katika siku kama ya leo miaka 249 iliyopita, Jane Austen, mwandishi mwanamke wa Uingereza alizaliwa.  

Hakuishi kwa zaidi ya miaka 42 kwani aliaga dunia 1817. Hata hivyo, Jane Austen alikuwa na taathira kubwa mno katika fasihi ya Kiingereza na hata Ulaya kwa ujumla.

Jane Austen

Siku kama hii ya leo miaka 161 alizaliwa George Santayana, mwanafalsafa na mwandishi wa Kihispania.

Akiwa na umri wa miaka 9 George Santayana alihajiri pamoja na familia yake na kuelekea Marekani. Baada ya kukamilisha masomo ya nmsingii na ya sekondari alijiunga na Chuo Kikuu cha Havard. Pamoja na hayo katika kipindi chake cha kuishi Marekani kwa muda wa miaka 41 alikuwa amejitenga na hakuwa na furaha.

Hatimaye mwaka 1913 Santayana aliekea barani Ulaya na kujifunza falsafa katika mataifa ya Uingereza na Ujerumani na kisha baadaye nchinii Italia.

George Santayana

Siku kama ya leo miaka 74 iliyopita katika siku kama ya leo ilianza harakati ya kupigania uhuru ya watu wa Cyprus kwa shabaha ya kuhitimisha ukoloni wa Waingereza kisiwani humo.

Kisiwa cha Cyprus kilichoko katika Bahari ya Miditerranean kiliwekwa chini ya utawala wa Kiothmania katika karne ya 16.

Mwaka 1925 Uingereza ilikiunganisha kisiwa hicho na makoloni yake na tangu wakati huo kulitokea mapigano baina wakazi wa kisiwa hicho yaani Waturuki na Wagiriki. Hatimaye Cyprus ilipata uhuru mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Wagiriki huku Waturuki wa kisiwa hicho wakidhibiti eneo la kaskazini la nchi hiyo. 

Katika siku kama hii ya leo miaka 33 iliyopita Kazakhstan ilijitangazia uhuru baada ya kudhihiri dalili za kusambaratika Urusi ya zamani.

Wakazaki ambao wanaunda jamii kubwa zaidi nchini humo na ambao ni kutoka makabila ya Waturki na Wamongoli, katika karne ya 17 miladia, waligawanyika katika sehemu tatu za tawala kubwa za kisultani. Mwanzoni mwa karne ya 18 taratibu waliwekwa chini ya udhibiti wa Warusi na wakati huo hususan katika karne ya 19, wakazaki hao wakiwa pamoja na watu wa maeneo mengine ya Asia ya kati, walijiunga na dini ya Kiislamu.

Miaka 33 iliyopita katika siku kama ya leo mwili wa Mhandisi Muhammad Javad Tondguyan, Waziri wa Mafuta wa wakati huo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulirejeshwa nchini Iran kutoka Iraq baada ya kupita miaka 11.

Waziri Tondguyan na maafisa wengine kadhaa wa wizara hiyo walitekwa nyara na wanajeshi wavamizi wa Iraq wakati walipokuwa katika ziara ya kutembelea visima vya mafuta vya kusini mwa Iran. Waziri huyo na wenzake walitekwa nyara mwezi mmoja baada ya Iraq kuvamia ardhi ya Iran.

Utawala wa Saddam wakati huo uliendelea kukanusha kutekwa nyara Mhandisi Tondguyan kwa muda fulani, lakini hatimaye ulikiri kumteka nyara waziri huyo wa zamani wa mafuta wa Iran.

Uchunguzi wa kidaktari na ushahidi uliotolewa na watu waliokuwa karibu na Waziri Muhammad Jawad Tondguyan ulithibitisha kwamba waziri huyo wa zamani wa mafuta wa Iran alikufa shahidi kutokana na kuteswa na askari jeshi wa utawala wa Baath wa Iraq. *

Mhandisi Muhammad Javad Tondguyan

Siku kama hii ya leo miaka 26 iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Paris ilimhukumu kifungo na kumtoza faini mwanafalsafa na msomi mashuhuri wa nchi hiyo, Roger Garaudy, kwa kosa eti la kukana jinai dhidi ya binadamu katika kitabu chake cha 'The Founding Myths of Israeli Politics'.

Katika kitabu hicho msomi huyo Mfaransa alithibitisha kisayansi na kwa hoja madhubuti kwamba Wazayuni walishirikiana na Manazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Vilevile amethibitisha kwa hoja na ushahidi kwamba, kwa shabaha ya kutaka kupata uungaji mkono wa kuunda dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina, Wazayuni walikuza na kutia chumvi kupita kiasi jinai zilizofanywa na Adolph Hitler dhidi ya Mayahudi.

Katika kitabu cha 'The Founding Myths of Israeli Politics' Profesa Garaudy anasema, idadi ya Mayahudi milioni 6 inayotajwa na Wazayuni kuwa iliuawa na Wajerumani wa zama za Hitler imetiwa chumvi kupita kiasi kwani jamii ya Wayahudi katika kipindi hicho haikuwa kubwa kiasi hicho.

Msomi huyo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo nchini Ufaransa kutokana na maoni yake, suala ambalo limethibitisha urongo wa madai ya demokrasia na uhuru wa maoni nchini Ufaransa.

Roger Garaudy