Jun 01, 2025 02:28 UTC
  • Jumapili, Mosi Juni, 2025

Leo ni Jumapili 5 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1446 Hijria inayosadifiana na Mosi Juni 2025 Miladia.

Katika siku kama ya leo miaka 365 iliyopita Mary Barrette Dyer, ambaye alikuwa mhubiri wa Quakerism huko Marekani, alinyongwa na mahakama ya Massachusetts kwa sababu za kidini. Wakati huo, sheria ya Massachusetts ilikataza Maquakers kuingia eneo hilo. Wafusi wa kundi hilo wanaojuulikana kama Quakers ni watu waliokuwa katika kundi la kihistoria la Kikristo la Kiprotestanti linalojulikana kama Jumuiya ya Kidini ya Marafiki. Quakerism iliibuka katika karne ya 16 na 17 kama jibu kwa hitilafu na vita vya kidini vilivyotokea huko Ulaya na vilevile uhasama na mizozo baina ya madhehebu ya Kikristo nchini Uingereza. George Fox alikuwa mmoja wa wahubiri mashuhuri wa kundi hilo. Kundi hili lilienea polepole katika ulimwengu wa Kikristo. Quakers waliamini katika kurahisisha shughuli za kidini na kwamba kanisa halipaswi kuwa na mchungaji maalumu na anayelipwa mshahara na kuwa kiunganishi na wasita kati ya Mungu na Mtume wake kwa upande mmoja, na watu wa kawaida kwa upande mwingine. Waliamini kuwa mahubiri na mafundisho ya Kikristo yanapaswa kufanywa kwa hiari na kila mtu mwenye ujuzi. ***

 

Miaka 111 iliyopita katika siku kama ya leo kwa mujibu wa kalenda ya Hijria, alizaliwa Sheikh Muhammad al-Ghazali, msomi, mwandishin na alimu mkubwa wa Kimisri. Muhammad al-Ghazali alizaliwa na kukulia katika familia iliyokuwa imeshikmana na dini. Kutokana na hima na idili kuubwa aliyokuwa katika masomo, Muhammad al-Ghazali alifanikiwa kuhitimuu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar akiwa na umri wa miaka 26 sambamba na kupata idhini ya kufundisha chuo hapo. Muhammad al-Ghazali ameandika vitabu visivyopungua 94. Msomii huyu alifanya hima na juhudi kubwa pia za kupigania umoja katika jami ya Kiislamu. Muhammad al-Ghazali aliaga dunia 20 Mfunguo Mosi Shawwal 1416 Hijria. ***

 

Siku kama ya leo miaka 85 iliyopita, alifariki dunia huko Najaf, Iraq Allamah Muhammad Hussein Gharawi Isfahani mashuhuri kkwa jiina la Kampani, mwanafalsafa, faqihi na mwanairfani mkubwa. Alizaliwa mwaka 1296 Hijria mjini Kadhimain nchini Iraq. Msomi huyo mkubwa alitabahari katika elimu za falsafa, tiba, irfan, historia, jiografia, mashairi na fasihi. Mbali na hayo Allamah Hussein Kampani alikuwa na fikra pevu na uwezo mkubwa wa kubainisha mambo. Msomi huyo ameandika vitabu kadhaa katika nyanja mbalimbali ikiwemo diwani ya mashairi akisifu viongozi wa Uislamu. ***

 

Siku kama ya leo tarehe Mosi Juni miaka 73 iliyopita, aliaga dunia John Dewey, msomi na mwandishi mashuhuri wa Marekani. Alihitimu falsafa katika Chuo Kikuu cha Vermont kabla ya kuwa na umri wa miaka ishirini, na baada ya kupata shahada ya uzamivu katika taaluma ya falsafa, alifundisha katika Chuo Kikuu cha Columbia. Dewey alibobea mno katika taaluma ya elimu na malezi. Dewey alifanikiwa kuandika vitabu vingi kuhusiana na elimu na malezi. Miongoni mwa vitabu mashuhuri vya msomi huyo ni pamoja na "How we Think", "The Public and its Problems" na "Freedom and Culture." John Dewey alifariki dunia mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka 93. ***

 

Miaka 43 iliyopita katika siku kama ya leo, Ustadh Seyyed Hossein Mirkhani, mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya ya Waandishi wa Hati Nzuri Iran na mwalimu mahiri wa wa maandishi ya Nastaliq, aliaga dunia baada ya juhudi za maisha yake yote katika fani ya calligraphy. Mwalimu Mirkhani alizaliwa mwaka wa 1286 Hijria Shamsia na akaanza kufanya mazoezi ya kuandika maandishi akiwa mtoto, na kufikia umri wa miaka kumi na moja alikuwa na mwandiko mzuri. Hossein Mirkhani alitumia miaka 30 ya maisha yake kuwaelimisha na kuwafunza wanafunzi wa kaligrafia. Mbali na ubunifu wake wa kisanii, Profesa Mirkhani pia alikuwa na maadili mema. Aliandika Kurani Tukufu kwa hati ya Nastaliq mara tatu wakati wa uhai wake.

 

Katika siku kama ya leo miaka 38 iliyopita, Chama cha Jamhuri ya Kiislamu, kikiwa chama kikubwa na kilichojumuisha watu wengi zaidi nchini Iran baada ya mapinduzi, kilivunjwa kwa pendekezo la wanachama wake. Chama cha Jamhuri ya Kiislamu kilianzishwa wiki moja baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Iran na Seyyed Mohammad Hosseini Beheshti, Seyyed Ali Khamenei (kiongozi wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran), Seyyed Abdolkarim Mousavi Ardebili, Akbar Hashemi Rafsanjani, na Dk. Muhammad Javad Bahonar.

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Jamhuri ya Kiislamu