Jumatatu, 21 Septemba, 2026
-
Leo Katika Historia
Leo ni Jumatatu 9 Mfunguo Saba Rabiuthani 1448 Hijria sawa na 21 Septemba 2026.
Miaka 287 iliyopita katika siku kama ya leo, Mkataba wa Belgrade ulitiwa saini kati ya Austria na utawala wa Othmania. Eneo la Austria lilikuwa chini ya udhibiti wa Uhispania na utawala wa Roma kwa miaka mingi, hadi watu wa nchi hii walipoibuka kama mamlaka huko Ulaya kuanzia 1700. Wakati huo huo, kulikuwa na vita vya mara kwa mara kati ya majeshi ya Austria na utawala wa Othmania, na mara kwa mara moja ya nchi hizo mbili ingeingia kwenye vita dhidi ya nyingine ili kunyakua eneo zaidi. Katika miaka ya mapema ya karne ya 18, Austria ilipohisi kuwa salama kwenye mipaka yake ya magharibi, iliweka mwelekeo wake wa kuteka maeneo ya mashariki.
@@@
Siku kama ya leo miaka 194 iliyopita, inayosadifiana na 21 Septemba 1832, aliaga dunia Sir Walter Scott, mwandishi wa riwaya, mshairi na mwanahistoria mahiri wa Uskochi. Alizaliwa 15 Agosti mwaka 1771 na baada ya kuhitimu masomo yake katika taaluma ya sheria, alifanya kazi ya uwakili kwa muda wa miaka 14. Hata hivyo, Sir Scott alikuwa na shauku na mapenzi makubwa na taaluma ya fasihi ya lugha.
@@@
Siku kama ya leo miaka 117 iliyopita, yaani 21 Septemba 1909, alizaliwa Dakta Osagyefo Kwame Nkrumah mwanasiasa na shujaa wa uhuru wa Ghana. Nkrumah alishiriki kikamilifu katika harakati za kupigania uhuru za wananchi wa Ghana dhidi ya mkoloni Muingereza. Baada ya kujipatia uhuru, kulijitokeza na kushuhudiwa njama kadhaa za kutaka kumuondoa madarakani na hata kumuua Nkrumah. Mwaka 1966 wakati Dakta Nkrumah akiwa safarini nchini China, Jenerali Joseph Ankrah alifanya mapinduzi na kuiondoa madarakani serikali Nkrumah. Mwanamapinduzi huyo aliaga dunia mwaka 1972 akiwa uhamishoni nchini Romania. Kwame Nkrumah alikuwa na nafasi muhimu katika kuasisiwa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM pamoja Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika OAU.
@@@
Katika siku kama ya leo miaka 32 iliyopita Bunge la Taifa la Ufaransa lilipasisha sheria iliyopiga marufuku vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu katika shule za nchi hiyo. Ufaransa ilipasisha sheria hiyo inayowazuia wanafunzi wa kike Waislamu kwenda mashuleni wakiwa na vazi la hijabu licha ya kudai kuwa ni kitovu cha demokrasia na uhuru. Baadaye sheria hiyo ilipanuliwa zaidi na kupiga marufuku vazi la hijabu katika vyuo vikuu na idara za umma. Wachambuzi wengi walikosoa vikali sheria hiyo wakisema inapingana na Katiba ya Ufaransa na Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu zinazosisitiza kuwa kila mtu ana uhuru wa kukubali na kutekeleza itikadi zake za kidini maadamu hazina madhara kwa watu wengine.
@@@
Miaka 39 iliyopita katika siku kama ya leo Septemba 21, 1987
Helikopta za kijeshi za Marekani zilishambulia meli ya huduma na lojistiki ya “Iran Ajr” katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Kufuatia vipigo mfululizo na kushindwa vibaya kwa utawala dhalimu wa Baath wa Saddam katika nyanja mbalimbali za mapambano ya nchi kavu, serikali ya Marekani katika msimu wa joto wa mwaka 1987 ilianzisha rasmi mashambulizi ya kijeshi dhidi ya meli za kibiashara, ndege za abiria, na vituo vya mafuta vya Iran ili kumpa nguvu na kumuokoa dikteta Saddam. Lengo kuu la ubeberu wa Marekani lilikuwa ni kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kusalimu amri na kusitisha vita kwa mujibu wa masharti na sera za kidhalimu zilizotaka kupandikizwa na madola ya Magharibi.
Katika mwendelezo wa siasa hizo za uadui, meli ya huduma na vifaa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyojulikana kama “Iran Ajr”, iliyomilikiwa na Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ilikuwa ikisafiri kwenye maji ya kimataifa ikitokea Bandar Abbas kuelekea Bandar Bushehr. Ghafla na bila onyo lolote la awali, meli hiyo ilishambuliwa kikatili na helikopta mbili za kijeshi za Marekani.
Katika uvamizi huo wa kinyama, mabaharia wanne wa meli hiyo waliuawa shahidi na wengine wanne wakajeruhiwa vibaya. Aidha, wanajeshi vamizi wa Marekani waliwateka nyara mabaharia wengine kumi (10) wa meli hiyo na kuwahamishia kwenye meli ya kivita ya kamandi ya jeshi la Marekani iliyokuwepo eneo hilo.
@@@
Na leo Septemba 21 ni Siku ya Alzheimer's Duniani.
Ugonjwa wa Alzheimer's hutokana na tatizo la neva na husababisha kufa taratibu kwa seli za ubongo na kuzuia matatizo ya kumbukumbu, kufikiri na katika mienendo ya mgonjwa. Pia, ugonjwa huu ndiyo sababu maarufu zaidi ya tatizo la akili la ugonjwa wa kupoteza fahamu, dementia. Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu mmoja ulimwenguni hugunduliwa na ugonjwa wa Alzheimer kila sekunde 68. Hivi sasa, zaidi ya watu milioni 50 duniani wanasumbuliwa na ugonjwa wa Alzheimer, na inatabiriwa kuwa idadi ya watu wenye tatizo la akili la dementia itafikia milioni 82 ifikapo 2030, na milioni 152 ifikapo 2050. Siku ya Alzheimer Duniani ni kampeni ya kimataifa ambayo hufanyika kila mwezi Septemba ili kuongeza ufahamu na kupinga unyanyapaa wa watu wenye tatizo hilo la akili. Kauli mbiu na mada ya kampeni ya Siku ya Alzheimer Duniani ya 2023 ni: "Never too early never too late" (Kamwe si mapema sana wala hujachelewe sana). Lengo la kaulimbiu hiyo ni kusisitiza jukumu kuu la kutambua sababu za hatari ya tatizo hilo na kuchukua hatua haraka za kuzuia hatari hiyo.