Nov 14, 2016 23:14 UTC
  • Jumanne, Novemba 15, 2016

Leo ni Jumanne tarehe 15 Safar 1438 Hijria sawa na tarehe 15, Novemba 2016.

Siku kama ya leo 386 iliyopita katika siku kama ya leo, sawa na tarehe 15 Novemba 1630 alifariki dunia Johannes Kepler mtarjumi na mtaalamu wa masuala ya nyota wa Ujerumani akiwa na umri wa miaka 59. Mtaalamu huyo wa masuala ya nyota baada ya kufanya utafiti wa kina alifanikiwa kuandika sheria ya Kepler, iliyoelezea mwenendo wa sayari na kugundua pia mwendo mduara dufu wa sayari ya Mercury.

Vasily Bartold

Siku kama ya leo, miaka 147 iliyopita, alizaliwa Vasily Bartold, mtaalamu maarufu wa masuala ya mashariki wa Russia huko katika mjini Saint Petersburg. Bartold alisoma na kuhitimu elimu katika chuo kidogo cha lugha za mashariki huko huko Saint Petersburg huku akiwa hodari katika lugha za Kifarsi, Kiarabu na Kituruki. Akiwa na umri wa miaka 27 alifikia daraja la mhadhiri msaidizi katika chuo hicho ambapo alifundisha historia ya mataifa ya mashariki, huku akifanya pia utafiti na utalii mkubwa katika uwanja huo. Aidha kwa kipindi fulani alifanya safari huko Turkmenistani kwa minajili ya kuendeleza utafiti wake na kubahatika kuandika utafiti huo katika kitabu chake alichokipa jina la 'Turkestani katika kipindi cha mashambulizi ya Mongoli.'

Susangerd

Na Miaka 36 iliyopita katika siku kama leo mji wa mpakani wa Susangerd huko kusini magharibi mwa Iran ulishuhudia mapambano kati ya wapiganaji wa Kiislamu na wanajeshi vamizi wa utawala wa zamani wa Iraq. Oparesheni hiyo ya kujihami ilifanywa na wapiganaji shupavu 200 wa Iran waliojumuisha wanajeshi wa ulinzi, wanamgambo wa kujitolea na idadi ya kadhaa ya wenyeji wa mji huo waliokuwa wakitumia silaha nyepesi dhidi ya jeshi vamizi la Saddam. Katika operesheni hiyo wapiganaji shupavu wa Iran chini ya uongozi wa shahidi Dakta Mustafa Chamran, walipambana vikali na kufanikiwa kuukomboa mji wa Susangerd.