Jun 27, 2018 02:17 UTC
  • Jumatano tarehe 27 Juni, 2018

Leo ni Jumatano tarehe 13 Shawwal 1439 Hijria sawa na Juni 27 , 2018

Siku kama ya leo miaka 23 iliyopita Sheikh Hamad bin Khalifa Aal Thani aliyekuwa mrithi wa Amir wa Qatar alifanya mapinduzi dhidi ya baba yake. Sheikh Hamad alimuondoa madarakani baba yake, Sheikh Khalifa bin Hamad Aal Thani wakati Amiri huyo wa zamani wa Qatar alipokuwa safarini nchini Uswisi. Sheikh Khalifa ambaye alikuwa kiongozi wa Qatar tangu mwaka 1972 alifanya jitihada kubwa za kurejea madarakani lakini hakufanikiwa. Nchi ndogo ya Qatar iko kusini mwa Ghuba ya Uajemi na inapakana na Saudi Arabia. Nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.

Sheikh Hamad bin Khalifa Aal Thani

Tarehe 6 Tir miaka 37 iliyopita Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ambaye wakati huo alikuwa mwakilishi wa Imam Ruhullah Khomeini katika Baraza Kuu la Ulinzi na pia Imam wa Ijumaa wa Tehran, alinusurika jaribio la kutaka kumuua lililofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la MKO. Magaidi hao walilipua bomu katika moja ya misikiti ya Tehran ambako Ayatullah Khamenei alikuwa akihutubia hadhara ya watu na kumjeruhi vibaya. Hata hivyo Imam Khamenei aninusurika jaribio hilo kwa njia ya kimiujiza na baadaye akashika usukani wa kuongoza jahazi la Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini. Ayatullah Ali Khamenei alijeruhiwa vibaya mkono wake wa kulia katika shambulizi hilo.

Ayatullah Ali Khamenei baada ya jaribio la mauaji

Siku kama ya leo miaka 41 iliyopita Djibouti ilipata uhuru baada ya kukoloniwa kwa miaka kadhaa na serikali ya Ufaransa. Djibouti ilikuwa chini ya mkoloni Mfaransa tangu mwaka 1896 ikijulikana kwa jina la Somalia ya Ufaransa. Hata hivyo Djibouti hatimaye ilipata uhuru wake baada ya miongo minane ya mapambano. Djibouti ni miongoni mwa nchi za mwisho kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Bendera ya Djibouti

Siku kama ya leo miaka 116 alifariki dunia Ayatullah Sheikh Muhammad Twaha, mmoja wa maulama wakubwa wa Kiislamu akiwa na umri wa miaka 83. Familia ya msomi huyo mkubwa inatokana na moja ya maulama mashuhuri wa Kiislamu. Aidha sheikh Twaha alizaliwa na mjini Najaf, Iraq huku akiwa mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Murtadha Answari, alim na faqihi mkubwa katika zama hizo. Aidha Aidha sheikh Twaha alitabahari katika elimu ya fiq’hi, usulu fiq’hi, hadithi na tafsiri ya Qur’ani Tukufu.