Dec 29, 2018 01:10 UTC
  • Jumamosi, 29 Desemba, 2018

Leo ni Jumamosi tarehe 21 Mfunguo Saba, Rabiu Thani 1440 Hijria mwafaka na tarehe 29 Desemba 2018.

Siku kama ya leo miaka 112 iliyopita, katiba ya Iran iliyokuwa imeandikwa na kuandaliwa na Bunge la kwanza la taifa ilitiwa saini na kupasishwa na mfalme wa wakati huo wa Iran Mozaffar ad-Din Shah Qajar. Katiba hiyo ilikuwa na vipengee 51 ambapo baadaye viliongezwa vipengee 107 kama vikamilisho. Katika kipindi cha miaka iliyofuata na katika zama za tawala mbalimbali hususan katika kipindi cha utawala wa kidikteta wa Kipahlavi, katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho ya kimsingi.  Akthari ya marekebisho hayo yalikuwa ni9 kwa madhara ya mamlaka ya wananchi na Uislamu.***

Katiba

 

Katika siku kama ya leo miaka 81 iliyopita, mkataba wa kupata uhuru Jamhuri ya Ireland ulitiwa saini baina ya viongozi wa wapigania jamhuri wa Ireland na utawala wa wakati huo wa Uingereza. Hata hivyo kutokana na kuanza Vita vya Pili vya Dunia, serikali ya Uingereza ilikataa kutekeleza mkataba huo. Baada ya vita hivyo, mnamo mwaka 1949, Jamhuri ya Ireland ya Kusini ilijitangazia rasmi uhuru wake toka kwa mkoloni Muingereza. Uhuru wa Ireland ilikuwa natija ya mapambano ya karne nane ya wapigania Jamhuri wa Ireland dhidi ya Uingereza. ***

Bendera ya Ireland

Miaka 88 iliyopita katika siku kama ya leo aliaga dunia Theodor Nöldeke msomi wa Kijerumani na mtaalamu wa mambo ya nchi za mashariki.  Alihitimu masomo yake katika taaluma ya teolojia, falsafa pamoja na lugha mbalimbali na kutunukiwa shahada ya uzamivu. Theodor Nöldeke alianza kufundisha Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 25 na kuifanya kazi hiyo kwa miaka mingi. Theodor Nöldeke alikuwa amebobea katika lugha za Kiarabu, KIifarsi, Kituruuki, Kigiriki, Kihispania na Kitaliano. ***

Theodor Nöldeke

Na katika siku kama ya leo miaka 69 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria aliaga dunia Ayatullah Muhammad Nahavandi alimu na msomi mkubwa wa Kiislamu. Ayatullah Nahavandi alikuwa mtoto wa alimu mkubwa Ayatullah Mirza Abdul-Rahim Nahavandi. Alizaliwa huko Najaf Iraq. Kama alivyokuwa baba yake, Muhammad Nahavandi alifanikiwa kukwea na kufikia daraja za juu za elimu na kuhesabiwa kuwa mmoja wa maulama wakubwa katika karne ya 14. Mbali na kufundishia, msomi huyo alikuwa pia mwandishi wa vitabu. ***

Ayatullah Muhammad Nahavandi