Dec 19, 2021 02:09 UTC
  • Jumapili tarehe 19 Disemba 2021

Leo ni Jumapili tarehe 14 Jamadil Awwal 1443 Hijria sawa na Disemba 19 mwaka 2021.

Katika siku kama ya leo miaka 234 iliyopita mwafaka na tarehe 19 Disemba 1787, nchi ya Kiafrika ya Sierra Leone iliunganishwa na Uingereza, baada ya kupita miaka 327 tangu ardhi ya nchi hiyo igunduliwe na wazungu. Sierra Leone iligunduliwa na mtalii wa Uhispania na kukoloniwa. Katika miaka ya kukoloniwa kwake na Uhispania, maelfu ya wanaume na wanawake wa Sierra Leone walichukuliwa watumwa na kwenda kuuzwa katika masoko ya Ulaya. Mwenendo huo uliendelea pia baada ya Waingereza kuishinda Uhispania na kuanza ukoloni wa Uingereza nchini humo. Mwaka 1961 Sierra Leone ilianza kujitawala na kuwa na utawala unaosimamiwa na jeshi na mwaka 1971 ikawa na utawala wa Jamhuri. 

Bendera ya Sierra Leone 

Miaka 115 iliyopita alizaliwa kiongozi wa Urusi ya zamani, katika familia maskini nchini Ukraine. Mwaka 1931, Leonid Brezhnev alijiunga na kuwa mwanachama wa chama hicho cha Kikomonisti. Brezhnev alitwaa uwaziri mkuu Russia na uongozi wa Chama cha Kikomonisti cha Urusi ya zamani mwaka 1964 wakati Nikita Khrushchev alipokuwa safarini nje ya nchi. Mashambulizi dhidi ya Czechoslovakia na kukaliwa kijeshi Afghanistan yalifanyika katika zama zake.

Leonid Brezhnev

 

Siku kama ya leo miaka 131 iliyopita, alifariki dunia mjini Tehran Haj Mulla Ismail Sabzevari, mpokezi wa hadithi na hatibu mkubwa wa karne ya 13 Hijria. Mulla Sabzevari alizaliwa katika eneo la Sabzevar lililoko kaskazini mashariki mwa Iran. Alijifunza falsafa kwa Mulla Hadi Sabzevari aliyekuwa mashuhuri kwa lakabu ya Mwanafalsafa wa Mashariki. Baadaye alihamia katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq kwa ajili ya elimu ya juu zaidi na kupata daraja ya ijtihad. Msomi huyo ameandika vitabu vingi kikiwemo kile cha "Majmaun Nurain" na "Nawadirul Aathar".

Miaka 31 iliyopita katika siku kama ya leo, Sadeq Ganji mwambata wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Lahore Pakistan alishambuliwa kwa risasi na vibaraka wa ubeberu wa kimataifa na kuuawa shahidi. Kwa karibu miaka minne Ganji alikuwa akitekeleza jukumu lake la kutangaza na kuziarifisha thamani aali za Kiislamu na kupanua uhusiano wa kiutamaduni baina ya wananchi wa Iran na Pakistan. Sadeq Ganjia aliuawa shahidi akiwa amekaribia kurejea hapa nchini baada ya hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na wana utamaduni na shakhsia wa kielimu na kifasihi wa Lahore Pakistan.

Shahidi Sadeq Ganji

Na siku kama ya leo Siku kama ya leo miaka 48 iliyopita, inayosadifiana na 19 Disemba 1972, kiongozi wa wakati huo wa Uganda Jenerali Idi Amin Dada aliwapatia wafanyakazi wa Kiingereza waliokuwa wakifanya kazi nchini humo makataa ya siku 12 wakubali kupunguziwa mishahara yao kwa asilimia 40 au waondoke nchini humo. Zoezi hilo liliwajumuisha karibu wafanyakazi 780 wa Kiingereza waliokuwa wakifanya kazi kwenye mashirika mbalimbali nchini Uganda.