May 07, 2022 23:48 UTC
  • Jumapili tarehe 8 Mei 2022

Leo ni Jumapili tarehe 6 Shawwal 1443 Hijria sawa na Mei 8 mwaka 2022.

Tarehe 8 ya kila mwezi Mei inatambuliwa kuwa siku ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu. Msalaba Mwekundu ni shirika la kimataifa ambalo liliundwa kwa ajili ya kutuliza machungu ya wanadamu na kulinda maendeleo ya sekta ya afya ya kijamii kwa mujibu wa mkataba wa Geneva, Uswisi hapo mwaka 1864 Miladia. Jean Henri Dunant raia wa Uswisi, alikuwa na nafasi kubwa katika kuundwa shirika hilo la kimataifa. Hii ni kwa kuwa mwaka 1862 alitoa pendekezo la kusaidiwa wagonjwa na majeruhi wa kijeshi, pendekezo ambalo lilipokelewa na asasi za masuala ya misaada ya kibinaadamu na kukubaliwa hapo baadaye na kongamano la kimataifa mjini Geneva mwaka 1864. Ni baada ya hapo ndipo shirika hilo la Msalaba Mwekundu likaundwa na kuanza kuenea duniani. Katika nchi za Kiislamu shirika hilo linaitwa kwa jina la Hilali Nyekundu.

روز صلیب سرخ و هلال احمر

Siku kama ya leo miaka 657 iliyopita, alifariki dunia Ibn Bardes, malenga na mpokeaji wa hadithi wa Kiislamu. Ibn Bardes alizaliwa huko Ba'labak moja kati ya miji ya Lebanon na kuelekea katika mji wa Damascus baada ya kukamilisha masomo yake ya awali, ambapo alinufaika na elimu ya maulamaa maarufu wa zama hizo. Msomi huyo wa Kiislamu alisafiri katika nchi mbalimbali za Kiislamu na akaanza kufundisha baada ya kukamilisha masomo yake. Alikuwa mashuhuri baina ya watu kwa kushikamana na dini, kutakasa nafsi na maadili mema. Miongoni mwa vitabu vya msomi huyo ni al Iilamu fii Wafayatil Aalam. ***

Tarehe 8 Mei 1794 aliuawa Antoine Laurent - de Lavoisier mtafiti, mvumbuzi na msomi wa Kifaransa na mmoja kati ya waanzilishi wa elimu ya kemia ya kisasa, baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kukatwa kichwa kutokana na amri ya utawala wa Kifalme baada ya mapinduzi ya Ufaransa. Lavoisier aligundua elementi zinazounda hewa katika utafiti wake. Baada ya hapo, mkemia huyo wa Kifaransa aliweza kuvumbua gesi ya oksijeni. Lavoisier anafahamika kama 'Baba wa Kemia ya Kisasa.

آنتوان لاوازیه

Siku kama ya leo miaka 204 iliyopita tatibu James Parkinson wa Uingereza aligundua ugonjwa wa Parkinson. Dalili kuu za ugonjwa huo ni zile zinazohusiana na kutetemeka sana kwa baadhi ya viungo vya mwili, kukaza misuli, mwendo wa pole yaani mtu hushindwa kutembea haraka pamoja na kupepesuka. Ugonjwa huo unasababishwa na baadhi ya matatizo ndani ya ubongo na hadi kufikia sasa tiba mujarabu ya maradhi hayo haijapatikana.

جیمز پارکینسون

Siku kama ya leo miaka 119 iliyopita mwafaka na tarehe 8 Mei 1902, mji wa Saint-Pierre uliteketea baada ya kulipuka volkano kwenye mlima Pelee kusini mwa Ufaransa. Watu wasiopungua elfu 30 walipoteza maisha yao kwenye maafa hayo yaliyochukua muda wa dakika tatu tu.

آتشفشان

Siku kama ya leo miaka 76 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 8 Mei 1945, vilimalizika Vita vya Pili vya Dunia baada ya Wanazi wa Ujerumani kusalimu amri bila ya masharti. Ujerumani ilianza kushindwa vita hivyo tokea mwaka 1943. Vita vya Pili vya Dunia vinahesabiwa kuwa vita vikubwa zaidi kutokea katika historia ya mwanadamu, kwani karibu watu milioni 55 waliuawa katika vita hivyo vilivyosababisha pia hasara kubwa.

پایان جنگ جهانی دوم

Na siku kama hii ya leo miaka 40 iliyopita mji wa Huweize ulioko kusini mwa Iran ulikombolewa katika operesheni kubwa iliyopewa jina la Baitul Muqaddas ya wanajeshi supavu wa Iran kutoka kwenye makucha ya jeshi vamizi la Saddam Hussein wa Iraq. Mji huo wa Huweize unatambuliwa kuwa moja kati ya nembo za ushujaa na ujasiri wa vijana wa Iran. Operesheni hiyo iliongozwa na Shahidi Alamul Huda na wenzake kadhaa waliopambana na maadui hadi tone la mwisho la damu zao katika miezi ya mwanzoni mwa uvamizi wa jeshi la Saddam Hussein dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ukombozi wa Huweize ulikuwa utangulizi wa ushindi mkubwa zaidi wa jeshi la Iran ya Kiislamu wa kukomboa mji wa Khorram-shahr.

شهید حسین علم الهدی، از فرماندهان حماسه هویزه