Familia Salama-4 (lishe)
Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nasi katika mfululizo huu mpya wa makala kuhusu Afya ya Familia. Makala hizi huangazia masuala mbali mbali ya afya ya familia kama vile lishe, mazoezi, madhara ya matumizi ya mihadarati, umuhimu wa mahaba katika familia n.k. Katika makala yetu hii ya nne ya mfululizo huu tutaangazia nafasi ya maziwa na bidhaa zake. Karibuni kujiunga nasi hadi mwisho.
Kati ya vyakula ambavyo hutumiwa kila siku na vina nafasi muhimu katika lishe ya mwanadamu ni maziwa na bidhaa zake.
Maziwa na bidhaa zake ni kundu asili la vyakula vyenye protein, mafuta, madini hasa phosphorous, kalsium, vitamini na amino asidi ambazo mwili hauwezi kuzalisha.
Bidhaa za maziwa hasa maziwa yenyewe ni tajiri kwa kalsium ambayo huwa na nafasi muhimu katika uundwaji na uimarishwaji meno na mifupa. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa kalsiumu ina faida chungu nzima na kwamba bidhaa za maziwa ni muhimu katika kupunguza unene na umetaboli au hali ya ujenzi na uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini.
Utafiti uliofanya Marekani hivi karibuni umebaini kuwa kiwango cha kalsimu inayotumiwa na mtu mnene huongekezeka kutoka miligrami 400 hadi 1000 pasina mabadiliko katika kiwango cha kalori. Baada ya mwaka moja kulishuhudiwa kupungua asilimia 4.9 ya mafuta mabaye mwilini miongoni mwa watu hawa.
Ingawa kalsiumu inaweza kupatikana kutoka katika vyakula vingine, maziwa ndio chanzo kikuu cha kalsiumu. Kwa mujibu wa Daktari Duane Alexander, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Watoto Marekani, anasema pasina kutumia maziwa kila siku, mwili hautaweza kupata kalsiumu. Aidha weledi wanasema bidhaa za maziwa zina nafasi muhimu katika afya ya ubongo na kuzuia kudidimia au kuzorota kiungo hiki muhimu cha mwili.
Maziwa na bidhaa za maziwa huzuia maradhi ya ubongo na kiakili.
Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, watoto walio na umri wa miaka mine hadi 8 huhitaji miligramu 800 za kalsiumu kila siku.
Kiwango hiki huongezeka hadi miligramu 1000 kwa mabarobaro. Aidha watu walio na umri wa zaidi ya miaka 51 wanahitaji miligramu 1300 za kalsium kila siku. Wanawake wanahitaji kalsium zaidi ya kundi lolote lile kwa sababu huwa wanakabiliwa na hatari zaidi ya kukabiliana na ugonjwa wa Osteoporosis au ugonjwa wa kuchezesha mifupa. Lactose ni carbohydrate kuu au sukari ambayo hupatikana katika maziwa. Kuna baadhi ya watu ambao miili yao haiwezi kustahamili lactose ambao Kiingereza hujulikana kama lactose intolerant. Kwa watu kama hawa wanashaurikiwa kutumia tembe za kasium kila siku chini ya usimamizi au ushauri wa daktari.
Watu ambao wenye tatizzo hilo la kutostahamili lactose mwilini huwa na kiwango duni cha lactase ambayo husaidia mchakato wa kufungua sukari katika maziwa wakati ikiwa mwilini.
Dalili za kutosahamili lactose ni kama vile kuhara, kichefuchefu, maumivu ya tumbo na gesi baada ya kutumia maziwa. Kutosathamili lactose au lactose intolerance huwakumba zaidi watu ambao wana ugonjwa wa tumbo na watafiti bado wanaendelea kuchgunza suala hilo.
@@@