Jumatatu, tarehe 13 Nachi, 2023
Leo ni Jumatatu tarehe 20 Shaaban 1442 Hijria inayosadifiana na tarehe 13 Machi 2023.
Katika siku kama ya leo miaka 1059 iliyopita alifariki dunia mwanahistoria na mtaalamu maarufu wa vitabu wa Kiislamu Ebn al Nadeem. Ibn Nadeem alipata umaarufu kutokana na kitabu cha "al Fehrest". Katika kitabu hicho Ibn Nadeem aliarifisha taaluma na elimu zote zilizokuwepo katika zama hizo na kutoa maelezo na wasifa wa wasomi mashuhuri wa elimu hizo. Kitabu hicho kinakusanya maelezo kamili kuhusu maulamaa na wasomi wa Kiislamu wa zamani hadi kufikia zama za Ibn Nadeem.

Siku kama ya leo miaka 290 iliyopita, yaani 13 Machi, 1733 alizaliwa Joseph Priestley, mkemia na mwanafizikia wa Uingereza. Msomi huyo aliishi katika kipindi kilichokuwa maarufu kama zama za dhahabu za kemia na elimu hiyo ilikuwa imepiga hatua. Katika uchunguzi na utafiti wake, Priestley alivumbua uvutaji pumzi katika mimea na gesi za oksijeni na haidrojeni. Joseph Priestley alifariki dunia mwaka 1804.
Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita sawa na tarahe 13 Machi 1948, Wazayuni waliokuwa na mfungamano na kundi la kigaidi la Haganah walishambulia kitongoji cha Wapalestina cha Husseiniyah katika eneo la kaskazini mwa Jalilah. Wazayuni hao licha ya kuwaua shahidi zaidi ya Wapalestina 60, waliharibu nyumba zao kadhaa. Hali kadhalika katika siku hiyo hiyo, wanajeshi wa Israel walizilipua kwa mabomu nyumba za Wapalestina katika eneo la 'Qatmuun' lililoko Baitul Muqaddas. Mauaji ya Waislamu wa Palestina yaliyofanywa na makundi ya kigaidi ya Israel yalitekelezwa kwa lengo la kutaka kutangaza uwepo wa utawala huo bandia kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina baada ya kuondoka vikosi vya majeshi ya Uingereza katika eneo hilo.
Siku kama ya leo miaka 40 iliyopita, inayosadifiana na 13 Machi 1983, Joshua Nkomo kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe alikimbilia nchini Uingereza akihofia usalama wa maisha yake. Nkomo ambaye alikiongoza chama cha Zimbabwe African People's Union (ZAPU) alisema kuwa, alilazimika kutoroka nchini Zimbabwe na kukimbilia Uingereza kwa kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Brigedi ya Tano ya jeshi la Zimbabwe kuizingira kambi yake iliyoko katika mji wa Bulawayo.
Na siku kama hii leo miaka 43 hayati Imam Ruhullah Khomeini alitoa amri ya kuundwa taasisi itakayokuwa ikishughulikia hali ya familia za mashahidi waliouawa katika harakati za Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Sehemu moja ya ujumbe huo ilisema: "Sisi sote tunajua kwamba, harakati ya Mapinduzi ya Kiislamu na ushindi wa mapinduzi hayo nchini Iran ni matunda ya kujitolea mhanga kwa matabaka ya wananchi na kuna udharura wa kuwaenzi na kuwajali zaidi mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu".
