-
Ramaphosa aziomba radhi nchi zilizoathirika na chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini
Sep 18, 2019 03:19Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametuma wajumbe katika nchi kadhaa za Kiafrika ambazo raia wake waliathirika zaidi na hujuma na mashambulio ya chuki dhidi ya raia wa kigeni kutoka Afrika akiziomba radhi serikali na wananchi wa nchi hizo.
-
Waafrika Kusini wajiunga na wageni katika maandamano ya kulaani 'xenophobia'
Sep 15, 2019 02:50Wananchi wazalendo wa Afrika Kusini wamejiunga na raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo, katika maandamano ya kulaani ghasia na mauaji yanayowalenga raia wa kigeni hususan Waafrika wanaoishi nchini humo.
-
Polisi Afrika Kusini: Kiwango cha mauaji nchini kinatisha
Sep 12, 2019 22:07Polisi nchini Afrika Kusini imeeleza wasiwasi wake kutokana na kukithiri kwa kiwango cha mauaji ya kiholela nchini humo.
-
Mamia ya raia wa Nigeria warejea nyumbani kutoka Afrika Kusini, Xenophobia yaendela kuchoche ghasia
Sep 12, 2019 02:31Mamia ya raia wa Nigeria waondoka nchini Afrika Kusini na kureje nchini kwao wiki moja baada ya kushadidi ghasia na mauaji yanayowalenga raia wa kigeni hususan Waafrika wanaoishi nchini humo.
-
Mamia ya raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini kurejeshwa nyumbani
Sep 10, 2019 03:11Serikali ya Nigeria inatazamiwa kuanza kuwarejesha nyumbani mamia ya raia wake wanaoishi nchini Afrika Kusini, kufuatia wimbi la ghasia na mashambulizi yaliowalenga wageni katika nchi hizo mbili.
-
Nigeria kumrudisha nyumbani balozi wake baada ya Afrika Kusini kufunga balozi zake nchini Nigeria
Sep 05, 2019 21:58Mgogoro wa kidiplomasia umezuka baina ya Afrika Kusini na Nigeria baada ya magenge ya watu kushambulia wageni huko Afrika Kusini, na matokeo yake wananchi wa Nigeria nao kushambulia vituo vya biashara vinavyomilikiwa na raia wa Afrika Kusini nchini mwao.
-
Afrika Kusini yakiri: "Afrophobia" inahusika katika hujuma zinazowalenga raia wa kigeni
Sep 05, 2019 08:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema kuwa tabia ya kujichukulia sheria mkononi dhdi ya raia wa nchi nyingine za Afrika wanaoishi nchini humo ni moja kati ya sababu za mashambulizi na hujuma zinazowalenga wafanyabiashara wa nchi za kigeni katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.
-
Wanigeria wenye hasira walipiza kisasi, wapora maduka ya Waafrika Kusini
Sep 05, 2019 00:09Mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni huko Johannesburg, Afrika Kusini yameibua hasira kote barani Afrika ambapo maduka yanayomilikiwa na mashirika ya Afrika Kusini yameporwa nchini Nigeria.
-
Watanzania waandamana mbele ya ubalozi wa A. Kusini, wataka ndege ya ATCL irejeshwe
Aug 28, 2019 07:52Umati wa watu umeandamana leo nje ya ofisi za ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, wakishinikiza mahakama ya nchi hiyo iachie huru ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) inayoshikiliwa nchini Afrika Kusini kufuatia kesi ya fidia inayomhusu mtu ajulikanaye kama Hermanus Steyn wa nchi hiyo na Serikali ya Tanzania.
-
Afrika Kusini yapiga marufuku bendera ya zama za utawala wa ubaguzi wa rangi
Aug 21, 2019 20:42Mahakama moja nchini Afrika Kusini imetoa hukumu ya kupiga marufuku kuonyeshwa hadharani bendera ya utawala uliopinduliwa wa ubaguzi wa rangi (apartheid) nchini humo.