Nov 05, 2019 14:11 UTC
  • Jacob Zuma
    Jacob Zuma

Kampuni ya kuuza silaha ya Thales ya Ufaransa imetangza kuwa, itaitaka Mahakama ya Juu ya Afrika Kusini ruhusa ya kukata rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa mwezi uliopita wa Oktoba iliyokataa kusitishwa kabisa kesi ya kula rushwa inayomkabili rais wa zamani wan chi hiyo, Jacob Zuma.

Kampuni ya Thales inatuhumiwa kwamba ilikubali kumpa Zuma dola elfu 34 kwa mwaka kwa kuilinda isichunguzwe kuhusiana na mauzo ya silaha yenye thamani ya dola bilioni mbili hapo mwaka 1999.

Tuhuma hizo ziliibuliwa miaka kumi iliyopita lakini ziliondolewa ili kumruhusu Jacob Zuma kugombea urais mwaka 2009. Mashtaka hayo yalirejeshwa tena baada ya Ofisi ya Mashtaka kutangaza kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumfikisha kizimbani.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma sasa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya rushwa baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kutaka kesi hiyo isitishwe kabisa.

Jacob Zuma

Uamuzi huo una maana kuwa, kutakuwa na uchunguzi zaidi kuhusu mpango wa ununuzi wa silaha wa mwaka wa 1999 ambapo Zuma anatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya kutengeneza silaha ya Ufaransa, Thales.

Zuma alikuwa rais kutoka mwaka wa 2009 hadi 2018, wakati alipolazimishwa kujiuzulu na chama tawala cha ANC kutokana na madai mengine tofauti ya rushwa.

Vilevile Zuma amesema kuwa atakata rufaa, suala mbalo linamaanisha kwamba yumkini kesi hiyo sasa ikaahirishwa hadi mwishoni mwa mwaka ujao wa 2020.  

Tags