Pars Today
Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab limetangaza kuwa limehusika na miripuko ya mabomu iliyoua watu 16 hapo jana Jumamosi katika nchi za Kenya na Somalia.
Kundi la kigaidi na ukufurishaji la al-Shabaab la Somalia limeteka mji mdogo lakini wa kistratajia ulioko kaskazini mashariki mwa eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland.
Katika kile kinachoonekana ni kuendelea kuparaganyika kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab, kamanda mwingine mwandamizi wa kundi hilo la ukufurishaji la Somalia amejisalimisha kwa serikali.
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa magaidi wa kundi la Al Shabab sasa wamebadilisha mbinu zao ili kuwawezesha kutekeleza mashambulizi mengi na hatari zaidi.
Watu waliojizatiti kwa silaha wanaosadikiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab wamewateka nyara madaktari wawili wa Cuba katika mpaka wa Kenya na Somalia.
Kiongozi wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Al Shabab amejisalimishwa kwa askari wa serikali ya Somalia katika mji wa Marka katika eneo la kusni mwa nchi hiyo la Lower Shabelle.
Kwa akali watu 15 wameuawa katika mripuko wa bomu lililokuwa limetegwa garini, nje ya hoteli na mikahawa katika eneo lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Kwa akali watu 15 wameuawa katika shambulizi la kigaidi la jana Jumamosi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Wanachama wasiopungua 16 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab wameuawa katika makabiliano baina ya kundi hilo na vikosi vya usalama katika eneo la Bar Sanguni na Jamame mkoani Lower Juba, kusini mwa Somalia.
Kwa akali watu wanane wameuawa nchini Somalia na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika soko la kuuza na kununua mifugo kusini magharibi mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.