Kiongozi mwandamizi wa kundi la kigaidi la Al Shabab ajisalimisha Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i52545-kiongozi_mwandamizi_wa_kundi_la_kigaidi_la_al_shabab_ajisalimisha_somalia
Kiongozi wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Al Shabab amejisalimishwa kwa askari wa serikali ya Somalia katika mji wa Marka katika eneo la kusni mwa nchi hiyo la Lower Shabelle.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 31, 2019 22:25 UTC
  • Kiongozi mwandamizi wa kundi la kigaidi la Al Shabab ajisalimisha Somalia

Kiongozi wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Al Shabab amejisalimishwa kwa askari wa serikali ya Somalia katika mji wa Marka katika eneo la kusni mwa nchi hiyo la Lower Shabelle.

Ahmed Abdi Ali, Kamanda wa Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA) katika eneo hilo amesema Ibrahim Mohammed Bitow alijisalimisha kwa askari wa serikali kufuatia oparesheni kali dhidi ya magaidi katika siku za hivi karibuni.

Kamanda Abdi Ali amesema baada ya oparesheni ya siu 14 dhidi ya magaidi wa al-Shabab katika mji wa Marka, Ibrahim aliamua kujisalimisha.

Ametoa wito kwa magaidi wengine wa al-Shabab katika eneo hilo wajisalimishe. Ibrahim ambaye alijisalimisha akiwa na walinzi wake alisema walipotoshwa kujiunga na kundi hilo la magaidi wakufurishaji na ametaka watu wa Somalia wawasamehe.

Magaidi wa al Shabab

Wakati huo huo wanajeshi wa Somalia walitekeleza oparesheni nyingine Ijumaa usiku kwa lengo la kuwatimua magaidi kutoka katika ngome yao mjini Barire kusini mwa Somalia.

Wanajeshi wa Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM) nao pia wameimarisha oparesheni zao dhidi ya magaidi wa al-Shabab kati na kusini mwa Somalia.