-
Makumi ya askari wauawa na kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi Burkina Faso
Oct 04, 2021 23:25Wanajeshi wasiopungua 14 wa serikali ya Burkina Faso wameuawa katika shambulizi la kigaidi huko kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Burkina Faso yaahidi marekebisho makubwa ya kiusalama ili kukabiliana na makundi ya wanamgambo
Aug 28, 2021 03:36Burkina Faso imetangaza kuwa itafanya mabadiliko katika vikosi vyake vya usalama ili kuweza kukabiliana na hujuma za makundi ya wanamgambo ambazo hadi sasa zimesababisha kuuliwa watu zaidi ya 1,400 na kupelekea wengine milioni 1.3 kuhama makazi yao. Makundi yenye silaha yamekuwa yakiendesha hujuma na kusababisha ukosefu wa amani huko Burkina Faso kwa miaka sita sasa.
-
Wanamgambo 17 wauawa kaskazini mwa Burkina Faso
Aug 13, 2021 19:30Wanamgambo 17 wameuawa baada ya kukabiliwa vikali na walinda usalama wa kujitolea huko kaskazini mwa Burkina Faso.
-
Kero la ugaidi; 50 wauawa Burkina Faso na Nigeria
Jun 15, 2021 22:05Jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa magaidi 25 wameuliwa katika operesheni iliyofanywa na askari wa jeshi hilo.
-
Burkina Faso yaahidi kuwafyekelea mbali wahusika wa mashambulizi ya karibuni
Jun 08, 2021 06:42Christophe Dabire Waziri Mkuu wa Burkina Faso ameahidi kuwa shambulizi lililofanywa hivi karibuni katika kijiji cha Solhan na wanamgambo wenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo na kuuwa watu 160 halitanyamaziwa kimya. Amesema shambulio hilo la kinyama halitapita hivihivi bila ya kuchukuliwa hatua wale wote waliohusika na jinai hiyo.
-
Makumi wauawa katika shambulio la watu wenye silaha Burkina Faso
Jun 05, 2021 22:04Watu waliokuwa na silaha wasiojulikana wameshambulia kijiji kimoja kaskazini mwa Burkina Faso na kuua makumi ya raia.
-
Mvua na mafuriko yaua na kujeruhi makumi nchini Burkina Faso
Sep 10, 2020 11:21Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa nchi hiyo inakabiliwa na janga la kimaumbile baada ya watu 13 kupoteza maisha kutokana na mafuriko, huku wengine 19 wakijeruhiwa.
-
HRW: Makaburi ya umati yagunduliwa kaskazini mwa Burkina Faso
Jul 08, 2020 03:38Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza habari ya kugunduliwa makaburi ya umati yenye maiti 180 katika mji wa Djibo, kaskazini mwa Burkina Faso.
-
HRW: Maafisa usalama wameua watu 31 nchini Burkina Faso
Apr 21, 2020 03:25Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linawatuhumu maafisa usalama wa Burkina Faso kuwa wameua makumi ya watu waliowakamata katika operesheni zao dhidi ya makundi ya kigaidi.
-
Mawaziri 4 Burkina Faso wapatwa na corona, idadi ya waathirika Afrika yaongezeka
Mar 21, 2020 07:23Mawaziri wanne wa serikali ya Burkina Faso wamepatwa na virusi vya corona huku kesi za maambukizi ya virusi hivyo barani Afrika zikiendelea kuongezeka.