• Rais wa China: Kadhia ya Palestina ndiyo kuu zaidi Asia Magharibi

    Rais wa China: Kadhia ya Palestina ndiyo kuu zaidi Asia Magharibi

    Jul 21, 2020 22:01

    Rais Xi jingping wa China amesema kadhia ya Palestina ndilo swala kuu zaidi hivi sasa katika eneo la Asia Magharibi.

  • Upinzani wa Russia na China kwa hatua za upande mmoja za Marekani

    Upinzani wa Russia na China kwa hatua za upande mmoja za Marekani

    Jul 18, 2020 22:18

    Siasa za kujichukulia hatua na maamuzi ya kipeke yake za Marekani katika miaka ya karibuni zimezusha hasira kali za viongozi wa nchi mbalimbali duniani; na aghalabu ya viongozi hao wamekosoa siasa hizo za Marekani na kusisitiza kutekelezwa siasa za ushirikiano wa pande kadhaa kwa maslahi ya pamoja. Katika msimamo wao wa karibuni wa kimataifa, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Russia na China wamekosa kuendelea siasa hizo za kivyake vyake za Marekani katika masuala ya kimataifa.

  • Zarif: Iran haitalipa taifa lolote hata shibri moja ya ardhi yake

    Zarif: Iran haitalipa taifa lolote hata shibri moja ya ardhi yake

    Jul 17, 2020 03:35

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria juu ya makubaliano ya miaka 25 ya ushirikiano kati ya Iran na China na kusisitiza kuwa, katu Jamhuri ya Kiislamu haitapeana hata shibri moja ya ardhi yake au kuipa nchi yoyote ile ikiwemo China, haki maalumu ya kutumia maeneo yake.

  • Watu 140 wafariki dunia kwa mafuriko China

    Watu 140 wafariki dunia kwa mafuriko China

    Jul 15, 2020 03:10

    Serikali ya China imetangaza kuwa watu takriban 140 wameaga dunia baada ya nchi hiyo kuathiriwa na mafuriko mabaya zaidi kuwahi kuikumba China katika kipindi cha zaidi ya miaka 30 nchini humo. Aidha watu milioni 38 wameathiriwa na mafuriko hayo na nyumba elfu 28 zimebomoka.

  • Iran yakanusha uvumi wa kuiuzia China kisiwa

    Iran yakanusha uvumi wa kuiuzia China kisiwa

    Jul 12, 2020 23:10

    Iran imekanusha uvumi kuwa imeiuzia China kisiwa chake cha Kish katika Ghuba ya Uajemi na hali kadhalika imekanusha madai kuwa imeafiki kuiuzia China mafuta ghafi ya petroli kwa bei rahisi.

  • New York Times: Mapatano ya Iran na China ni pigo kubwa kwa Trump

    New York Times: Mapatano ya Iran na China ni pigo kubwa kwa Trump

    Jul 12, 2020 08:40

    Gazeti la New York Times limechapisha sehemu ya waraka wa mapatano ya ushirikiano wa Iran na China na kusema kuwa mapatano hayo ni pigo kubwa kwa sera dhidi ya Iran za Rais Donald Trump wa Marekani.

  • Russia na China zalipigia kura ya veto azimio linalokiuka mamlaka ya kujitawala ya Syria

    Russia na China zalipigia kura ya veto azimio linalokiuka mamlaka ya kujitawala ya Syria

    Jul 10, 2020 23:25

    Russia na China zimelipigia kura ya veto azimio lililotaka kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa nchini Syria bila ya idhini ya serikali kuu ya nchi hiyo.

  • China yaonya kuhusu mripuko wa homa ya mapafu iliyo hatari zaidi ya Covid-19 Kazakhstan

    China yaonya kuhusu mripuko wa homa ya mapafu iliyo hatari zaidi ya Covid-19 Kazakhstan

    Jul 10, 2020 03:38

    Ubalozi wa China nchini Kazakhstan umetoa indhari juu ya mripuko wa homa ya mapafu isiyojulikana (pneumonia) na ambayo ni hatari zaidi kuliko ugonjwa wa Covid-19.

  • Kujiondoa rasmi Marekani katika Shirika la Afya Duniani WHO

    Kujiondoa rasmi Marekani katika Shirika la Afya Duniani WHO

    Jul 09, 2020 04:51

    Msimamo wa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ni kupuuza, kukosoa, kutoa vitisho na hatimaye kujitoa katika mashirika ya kimataifa na hasa yale yanayopinga matakwa na maslahi haramu ya nchi hiyo na ya washirika wake na hasa utawala haramu wa Israel.

  • Mousavi: Viongozi wa Iran na China wameazimia kustawisha uhusiano wa kistratejia

    Mousavi: Viongozi wa Iran na China wameazimia kustawisha uhusiano wa kistratejia

    Jul 08, 2020 19:42

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa kwa mujibu wa mapatano ya mwaka 2016 kati ya Marais wa Iran na China, nchi mbili ziliweka wazi irada na azma yao ya kisiasa ya kustawisha na kupanua zaidi ushrikiano wa kistratejia na kuandaa ramani ya njia ya miaka 25 kati ya Tehran na Beijing ili kutayarisha uwanja mzuri wa ustawi wa pande zote katika uhusiano wa kisiasa na kiuchumi katika miaka ijayo.