-
Raisi: Marekani ifunguliwe mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na Daesh
Nov 04, 2019 03:13Mkuu wa Idara ya Mahakama za Iran amesema kuwa, Wamarekani wamekiri rasmi kwamba ndio walioanzisha kundi la kigaidi la Daesh, kwa msingi huo wanapaswa kufunguliwa mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na kundi hilo.
-
Raisi: Marekani ifikishwe kizimbani kwa kuasisi kundi la kigaidi la ISIS
Nov 03, 2019 12:35Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Marekani imekiri rasmi kuwa ilianzisha kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) na kwa msingi huo inapaswa kufikishwa kizimbani kujibu mashtaka kuhusu jinai za kundi hilo."
-
Sisitizo la Lavrov juu ya mchango wa Marekani katika kudhihiri al Baghdadi na Daesh
Nov 03, 2019 02:32Baada ya kuanza mgogoro wa Syria hapo mwaka 2011 na vita vilivyosababishwa na mgogoro huo, Marekani ilikuwa na nafasi muhimu na kuu katika kuundwa na kujitokeza makundi ya kigaidi nchini humo hususan kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh; suala ambalo Washington imefanya jitihada kubwa za klificha kwa kuanzisha kile ilichodai ni muungano wa kupambana na Daesh.
-
DAESH (ISIS) lathibitisha kuuawa Abu Bakr al-Baghdadi, latangaza kiongozi wake mpya
Nov 01, 2019 02:52Kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) limethibitisha na kukiri kuwa kiongozi wa kundi hilo Abu Bakr al- Baghdadi ameuliwa.
-
Marekani yadai imeitupa baharini maiti ya Abu Bakr al Baghdadi
Oct 29, 2019 16:36Mkuu wa majeshi ya Marekani amedai kuwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh, Abu Bakr al Baghdadi umetupwa bahaini baada ya kuthibitishwa kuwa wake kupitia kipimo cha vinasaba (DNA).
-
Abu Bakr al Baghdadi, Daesh na maafa yaliyosababishwa na kundi hilo
Oct 29, 2019 02:53Hatimaye kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh, Abu Bakr al Baghdadi ameangamizwa, na Abdullah Qardash aliyekuwa afisa wa jeshi la Saddam Hussein nchini Iraq ameteuliwa na kundi hilo kuwa kiongozi mpya wa Daesh.
-
Mousavi: Iraq na Syria ziliisambaratisha kitambo ISIS kwa msaada wa Iran
Oct 28, 2019 12:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) lilisambaratishwa na Iraq na Syria muda mrefu umepita, kwa msaada wa kilojistiki wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Ripoti: Al-Baghdadi aliponzwa na taarifa muhimu zilizotolewa na msaidizi wake wa karibu
Oct 28, 2019 08:03Ismael al-Ethawi, mmoja wa wasaidizi wa karibu wa kiranja wa kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) Abubakar al-Baghdadi alivipatia vyombo vya intelijensia vya Iraq taarifa mnamo mwezi Februari mwaka 2018 kuhusu namna mpangaji huyo wa mashambulio kadhaa ya kigaidi alivyofanikiwa kukwepa kutiwa nguvuni kwa muda wa miaka kadhaa.
-
Kuangamizwa al Baghdadi na njama za Marekani za kujifanya inapambana na Daesh
Oct 28, 2019 05:59Marekani pamoja na waitifaki wake wa Kiarabu na Kimagharibi ndio waliolianzisha, kulitia nguvu na kuliunga mkono kwa kila namna na hali na mali; genge la kigaidi na la ukufurishaji la Daesh (ISIS) kwa shabaha ya kuiangusha serikali halali ya Syria.
-
Abubakr al-Baghdadi, kiongozi wa Daesh auawa
Oct 27, 2019 07:38Afisa mmoja wa Pentagon nchini Marekani amesema kuwa Abubakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ameuawa katika operesheni ya siri iliyotekelezwa kaskazini magharibi mwa Syria.