Raisi: Marekani ifunguliwe mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57042-raisi_marekani_ifunguliwe_mashtaka_kutokana_na_jinai_zilizofanywa_na_daesh
Mkuu wa Idara ya Mahakama za Iran amesema kuwa, Wamarekani wamekiri rasmi kwamba ndio walioanzisha kundi la kigaidi la Daesh, kwa msingi huo wanapaswa kufunguliwa mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na kundi hilo.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Nov 04, 2019 03:13 UTC
  • Sayyid Ebrahim Raisi
    Sayyid Ebrahim Raisi

Mkuu wa Idara ya Mahakama za Iran amesema kuwa, Wamarekani wamekiri rasmi kwamba ndio walioanzisha kundi la kigaidi la Daesh, kwa msingi huo wanapaswa kufunguliwa mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na kundi hilo.

Sayyid Ebrahim Raisi amesema kuwa Marekani ndiyo mwanzishi na mfadhili mkuu wa ugaidi duniani na kuongeza kuwa, wanasheria kote duniani na jumuiya huru za kutetea haki za binadamu zinapaswa kutoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya wakiukaji wa haki za binadamu. 

Raisi amesema kuwa mienendo iliyodhidi ya binadamu ya Marekani ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kupindukia, kutungua ndege ya abiri ya Iran na mauaji ya raia wasio na hatia yoyote wa Palestina na Yemen ni jinai zinazopaswa kushughulikiwa katika mahakama ya kimataifa. 

Mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa ikitetea haki za binadamu na kuongeza kuwa, suala hilo ni fursa nzuri inayoweza kutumiwa kwa ajili ya kuwatangazaia walimwengu kazi nzuri inayofanywa na Iran katika kutetea haki za bindamu.