-
HRW: Daesh wanatumia silaha za kemikali wakikimbia Mosul
Nov 12, 2016 04:20Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh wanatumia silaha za kemikali kaskazini mwa mji wa Mosul nchini Iraq.
-
UN: Daesh imeua makumi ya raia eneo la Hammam al-Alil, Iraq
Nov 12, 2016 00:37Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limeua kwa umati makumi ya raia wa Iraq katika eneo la Hammam al-Alil lililoko kilomita 17 kutoka kwenye mji unaozingirwa na vikosi vya jeshi la Iraq wa Mosul.
-
Putin: Syria ni uwanja wa kudhihirisha azma ya dunia ya kupambana na ugaidi
Nov 10, 2016 03:35Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, Syria ni medani ya kuonesha azma na ustahiki wa jamii ya kimataifa kwa ajili ya kupambana na ugaidi.
-
Manowari za Russia kushambulia magaidi Aleppo, Syria
Nov 09, 2016 04:37Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema hii leo vikosi vyake vya majini vitaanzisha operesheni kali ya kuangamiza magaidi katika mji wa Aleppo nchini Syria.
-
Kaburi la umati lagunduliwa karibu na Mosul nchini Iraq
Nov 08, 2016 04:15Vikosi vya serikali ya Iraq vimegundua kaburi la umati karibu na mji wa Mosul ambao kwa sasa unashuhudia makabiliano makali kati ya vikosi hivyo na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh/ISIS.
-
Saudi Arabia inaunga mkono ugaidi barani Afrika
Nov 08, 2016 03:48Gazeti la Washington Post la Marekani limeandika makala kuhusu kuenea Uwahhabi nchini Nigeria na kuongeza kuwa, utawala wa Saudi Arabia unaaunga mkono viongozi wa Mawahhabi ili waweze kueneza Uwahhabi nchini humo na kote barani Afrika.
-
Makumi ya maelfu ya watu waukimbia mkoa wa Nainawa, Iraq
Nov 05, 2016 23:14Kamati ya Wahajiri ya Bunge la Iraq imetangaza kuwa, karibu watu 29 elfu wameukimbia mkoa wa Nainawa tangu ilipoanza operesheni ya kuukomboa mji wa Mosul, makao makuu ya mkoa huo.
-
Jeshi la Iraq lakomboa wafungwa 45 mikononi mwa Daesh Mosul, makumi ya magaidi waangamizwa
Nov 05, 2016 09:15Kamanda wa jeshi la Iraq katika mkoa wa Nainawa (Nineve) nchini Iraq, ametangaza kuwa jeshi la serikali kwa kushirikiana na harakati ya wananchi, limefanikiwa kuwakomboa wafungwa 45 waliokuwa wakishikiliwa na genge la kigaidi la Daesh (ISIS) magharibi mwa Mosul.
-
Russia: Marekani inalenga makazi ya raia Mosul, Iraq
Nov 04, 2016 01:07Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa mashambulizi ya ndege za kivita za Marekani na washirika wake yanalenga zaidi makazi ya raia katika mji wa Mosul nchini Iraq.
-
Johnson: Magaidi 130 wa Uingereza wameuawa nchini Syria
Nov 04, 2016 00:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema kuwa, raia 130 wa nchi hiyo wanachama katika kundi la kigaidi la Daesh wameuawa nchini Syria.