Manowari za Russia kushambulia magaidi Aleppo, Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i19114-manowari_za_russia_kushambulia_magaidi_aleppo_syria
Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema hii leo vikosi vyake vya majini vitaanzisha operesheni kali ya kuangamiza magaidi katika mji wa Aleppo nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 09, 2016 04:37 UTC
  • Manowari za Russia kushambulia magaidi Aleppo, Syria

Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema hii leo vikosi vyake vya majini vitaanzisha operesheni kali ya kuangamiza magaidi katika mji wa Aleppo nchini Syria.

Shirika la habari la Russia Today limeripoti kuwa, manowari za Russia zikiongozwa na meli mbili za kijeshi zinazoitwa 'Admiral Kuznetsov' na 'Peter the Great' zitatekeleza hujuma hiyo katika maeneo ambayo hayana raia, viungani mwa Aleppo.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia imeongeza kuwa, ndege za kivita za nchi hiyo vilevile zitafyatua makombora  kutokea kwenye meli hizo za kijeshi. Aidha operesheni hiyo ya baharini ya jeshi la Russia itazihusisha nyambizi katika kuwaangamiza matakfiri wa kundi la kigaidi la Daesh/ISIS.

Manowari ya Russia

Jeshi la Syria likisaidiwa na vikosi vya jeshi la anga la Russia hivi karibuni lilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi kwa minajili ya kuwatimua magaidi katika mji wa Aleppo ambapo hadi sasa maelfu ya magaidi wa Daesh na wa makundi mengine ya kigaidi wameuliwa na wengine karibu 2500 kujeruhiwa.

Mashambulizi ya anga mjini Aleppo

Mbali na operesheni hiyo ya kuukomboa mji huo wa kistrataji, operesheni nyingine ya kuukomboa mji wa Raqqah iliyopewa jina la "Hasira za Furat" iliyoanza usiku wa Jumamosi Novemba 5, inaendelea kwa kuwashirikisha askari karibu 30 elfu.