-
Kuanza mwenendo wa kusailiwa Trump
Jan 11, 2021 09:41Hujuma ya tarehe 6 mwezi huu ya wakereketwa na wafuasi sugu wa Rais Donald Trump katika Congress ya Marekani imezua radiamali kali katika nchi hiyo na sasa Wamarekani wanataka rais huyo achukuliwe hatua za kisheria, na tayari Wademokrat wameanzisha mwenendo wa kusailiwa kwake bungeni.
-
Wazayuni waongeza kasi ujenzi wa vitongoji vya walowezi siku za mwisho za Trump madarakani
Jan 11, 2021 04:32Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imetangaza kuwa, katika siku hizi za mwisho za kukata roho serikali ya Donald Trump huko Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel umeongeza maradufu kasi ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ulizowapora Wapalestina.
-
Pence abariki mchakato wa kuuzuliwa Trump
Jan 10, 2021 05:13Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa kuna uwezekana kutumia kifungu cha 25 cha Katiba kwa ajili ya kumuuzulu Rais Donald Trump.
-
Akthari ya Wamarekani wanataka Trump aondolewe madarakani haraka
Jan 09, 2021 09:24Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa nchini Marekani yanaonyesha kuwa, baada ya jengo la Kongresi kushambuliwa na kuvamiwa na wafuasi wa Rais Donald Trump, Wamarekani wengi wanataka kiongozi huyo aondolewe madarakani haraka.
-
Nasrallah: Wamarekani wamefahamu hatari ya Trump, yeye ni mfano halisi wa uistikbari
Jan 08, 2021 23:26Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema matukio ya hivi karibuni katika Bunge la Congress nchini Marekani yamepelekea Wamarekani wafahamu hatari ya rais wa nchi hiyo anayeondoka Donald Trump. Aidha amesema matukio hayo ni mfano halisi na wa wazi wa ubeberu na uistikbari wa Marekani.
-
Zarif akosoa undumakuwili wa Wamagharibi mkabala wa mienendo ya Trump
Jan 08, 2021 23:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali undumakuwili wa nchi za Magharibi ambazo hivi sasa zinakosoa mienendo ya kukanyaga utawala wa sheria ya Rais Donald Trump wa Marekani, licha ya kufuata kibubusa sera zake za kibeberu katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
-
Mahakama ya Iraq yaamuru Trump akamatwe kwa mauaji ya makamanda wa muqawama
Jan 07, 2021 23:14Mahakama ya Ar-Rasaafah nchini Iraq inayofuatilia kesi ya mauaji ya makamanda wa muqawama Luteni Jenerali Qassem Suleimani na Abu Mahdi al-Muhandis imetoa waranti wa kukamatwa rais wa Marekani Donald Trump.
-
Makombora yenye shabaha kali ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran ndilo tishio kubwa zaidi kwa Israel 2021
Jan 07, 2021 23:13Kituo cha tafiti za usalama wa ndani cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kimetangaza kuwa tishio kubwa zaidi kwa utawala huo katika mwaka huu wa 2021 ni makombora yenye shabaha kali ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran.
-
Hatimaye Trump asalimu amri, aahidi mapokezano ya madaraka yatafanyika kulingana na utaratibu
Jan 07, 2021 13:39Baada ya Kongresi ya Marekani kuthibitisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais, hatimaye rais wa nchi hiyo Donald Trump ametangaza kuwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa rais mteule utafanyika kama ulivyo utaratibu rasmi.
-
Rouhani: Demokrasia ya nchi za Magharibi ni dhaifu na isiyo na misingi
Jan 07, 2021 08:26Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema matukio ya hivi karibuni nchini Marekani ikiwa ni pamoja na kuvamiwa jengo la Bunge la Congress yanaashiria udhaifu na kutokuwa na msingi demokrasia ya nchi za Magharibi.