Asilimia 80 ya Wamarekani wanaamini nchi yao inasambaratika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65770-asilimia_80_ya_wamarekani_wanaamini_nchi_yao_inasambaratika
Uchunguzi mpya wa maoni umebaini kuwa, karibu asilimia 80 ya Wamarekani wote wanaamini kuwa nchi yao inaelekea kusambaratika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 15, 2021 01:06 UTC
  • Asilimia 80 ya Wamarekani wanaamini nchi yao inasambaratika

Uchunguzi mpya wa maoni umebaini kuwa, karibu asilimia 80 ya Wamarekani wote wanaamini kuwa nchi yao inaelekea kusambaratika.

Uchunguzi huo wa maoni umefanywa na shirika la Axios-Ipsos na umefanyika wiki moja baada ya wanamgambo watiifu kwa rais anayeondoka Donald Trump kuvamia jengo la Bunge la Congress na kupelekea vikao kusitishwa kwa muda wa masaa sita. Aidha watu watano waliuawa katika tukio hilo ambalo linaendelea kuitikisa Marekani.

Shirika la Axios-Ipsos limesema limewahoji watu 1,000 kunazia Jumatatu hadi Jumatano na kubaini kuwa, aghalabu wanaaamini kuwa 'Marekani inaelekea kusambaratika."

Aidha uchunguzi huo wa Axios-Ipsos umebaini kuwa Wamarekani  wanaotaka Trump aondolewe madarakani kabla hajamaliza muhula wake uliobakia siku chache kufika ukingoni wameongezeka kwa asilimia tano.

Wanamgambo wa Trump wakiwa wamevamia jengo la Bunge la Congress

Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kuwa asilimia 56 ya Wamarekani wanaafiki pendekezo la Trump kuondolewa madarakani mara moja katika hali ambayo idadi hiyo ilikuwa asilimia 51 wiki iliyopita.